Pata taarifa kuu
MAUAJI-HAKI

Burkina Faso: Mkuu wa majeshi anaonya juu ya hatari ya kuongezeka kwa tishio la kigaidi

Nchini Burkina Faso, Mkuu wa Majeshi nchini Mali anatoa wito kwa vikosi vya ulinzi na usalama kuwa macho. Katika taarifa, Brigedia Jenerali Célestin Simporté anapendekeza kuweka machapisho mbalimbali ya usalama kwenye tahadhari ya kudumu, kwa sababu kulingana na Mkuu wa majeshi, ongezeko la hatari ya mashambulizi ya kujitoa muhanga ni jambo la kuogopwa.

Jeshi la Burkina Faso likiwa kwenye doria mnamo Septemba 29, 2015.
Jeshi la Burkina Faso likiwa kwenye doria mnamo Septemba 29, 2015. AFP PHOTO / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Mkuu wa Majeshi, mashambulizi katika maeneo ya mijini yanapaswa kuogopwa. Brigedia Jenerali Célestin Simpora kwa hivyo anatoa wito wa kuongezeka kwa umakini.

Anapendekeza ongezeko la kiwango cha tahadhari, doria kila mara, ukaguzi na upekuzi wa watu na magari, pamoja na uimarishaji wa vifaa vya vikwazo kwenye barabara. Pia anatoa wito wa kufuata madhubuti kwa hatua zilizowekwa.

Tahadhari hii inajiri wiki moja baada ya mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi yaliyolenga kikosi cha kijeshi, msikiti na kanisa. Siku chache zilizopita, jeshi la Burkina Faso liliwaangamiza magaidi kadhaa, akiwemo mwanachama mkuu wa kundi linalotetea Uislamu na Waislamu.

Hassane Idrissa Boly amewasilishwa kama mmoja wa viongozi wakuu wa magaidi wanaoendesha shughuli zao huko Mouhoun, katika jimbo la kaskazini-magharibi mwa Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.