Pata taarifa kuu

Nigeria: Gavana wa Lagos atangaza hatua za kupunguza gharama ya maisha

Gavana wa Lagos ametangaza siku ya Alhamisi msururu wa hatua za kupunguza gharama ya maisha kwa wakaazi wa mji mkuu wa uchumi wa nchi hiyo katika muktadha wa mfumuko wa bei uliokithiri na vitisho vya maandamano ya kiraia.

Hali ngumu ya maisha ilisababisha maandamano katika miji kadhaa mwezi Februari, ikiwa ni pamoja na Suleja, karibu na mji mkuu Abuja, Minna, jimbo la Niger, na Kano, mji wa pili nchini humo. Siku ya Jumatatu, mamia ya waandamanaji walikusanyika Ibadan, kusini magharibi mwa Nigeria, kudai "kukomeshwa kwa umaskini".
Hali ngumu ya maisha ilisababisha maandamano katika miji kadhaa mwezi Februari, ikiwa ni pamoja na Suleja, karibu na mji mkuu Abuja, Minna, jimbo la Niger, na Kano, mji wa pili nchini humo. Siku ya Jumatatu, mamia ya waandamanaji walikusanyika Ibadan, kusini magharibi mwa Nigeria, kudai "kukomeshwa kwa umaskini". © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Babajide Sanwo-Olu, gavana wa Jimbo la Lagos, ambalo mji mkuu wake una wakazi milioni 20, ameeleza wazi mbele ya vyombo vya habari siku ya Alhamisi hatua zinazolenga kupunguza matumizi ya wakazi. Miongoni mwa hatua hizo, wiki ya kazi ilipungua hadi siku tatu kwa watumishi wa umma, punguzo la 25% la bei za tikiti za usafiri wa umma, na kufunguliwa kwa masoko 42 ya Jumapili kwa bei za ushindani. Gavana huyo ametangaza kwamba "wanawake wajawazito 50,000" wataondolewa gharama za afya kila mwaka.

Matangazo haya, yaliyorejelewa kwenye ukurasa wa X wa gavana, yanakuja wakati shirikisho la vyama vya wafanyakazi la Nigeria Labor Congress (NLC) limeitisha wiki hii kwa siku mbili za maandamano ya kitaifa tarehe 27 na 28 Februari.

Hali ngumu ya maisha ilisababisha maandamano katika miji kadhaa mwezi Februari, ikiwa ni pamoja na Suleja, karibu na mji mkuu Abuja, Minna, jimbo la Niger, na Kano, mji wa pili nchini humo. Siku ya Jumatatu, mamia ya waandamanaji walikusanyika Ibadan, kusini magharibi mwa Nigeria, kudai "kukomeshwa kwa umaskini".

Ingawa maandamano haya bado hayajazaa mikusanyiko mikubwa, serikali ya Nigeria hata hivyo iko chini ya shinikizo. Alipoingia madarakani Mei 2023, Rais Bola Tinubu alikomesha ruzuku ya mafuta na udhibiti wa sarafu, hali iliyosababisha kupanda mara tatu kwa bei ya petroli na kupanda kwa gharama ya maisha, naira (fedha za Nigeria) kupoteza thamani yake kwa kasi dhidi ya dola.

Rais wa Nigeria amerudia kuwataka wakazi kuwa na subira, akithibitisha kuwa mageuzi yake ya kiuchumi yatavutia wawekezaji wa kigeni na kuanzisha upya uchumi. Kiwango cha mfumuko wa bei nchini Nigria kilikaribia 30% mwezi Januari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.