Pata taarifa kuu

Nigeria: Mwanzilishi wa ECOWAS atoa wito wa kuondolewa vikwazo dhidi ya serikali za kijeshi

Mmoja wa waanzilishi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ametoa wito siku ya Jumatano kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya nchi za Afrika Magharibi zinazoongozwa na serikali za kijeshi kutokana na mapinduzi ya kijeshi, mbinu ya mkutano wa kilele usio wa kawaida uliopangwa kufanyika Jumamosi huko Abuja.

Bendera ya ECOWAS ikiwa na bendera za wanachama wakati wa mkutano wa pili usi wa kawaida kuhusu hali ya kisiasa nchini Burkina Faso, mjini Accra, Ghana, Februari 3, 2022.
Bendera ya ECOWAS ikiwa na bendera za wanachama wakati wa mkutano wa pili usi wa kawaida kuhusu hali ya kisiasa nchini Burkina Faso, mjini Accra, Ghana, Februari 3, 2022. © Nipah Dennis / AFP
Matangazo ya kibiashara

ECOWAS imetumbukia katika mzozo ambao haujawahi kushuhudiwa tangu kutangazwa mwishoni mwa mwezi wa Januari na Mali, Niger na Burkina Faso ya kujiondoa katika jumuiy hii ya kikanda. Eneo hilo pia limetikiswa hivi karibuni na uamuzi wa ghafla wa Rais Macky Sall wa kuchelewesha uchaguzi wa rais nchini Senegal.

ECOWAS "inakabiliwa na tishio la mgawanyiko", ameonya Jenerali Yakubu Gowon, mkuu wa zamani wa Nigeria (1966-1975), wakati wa mkutano ulioandaliwa na kambi hiyo katika mji mkuu wa Nigeria. Amewataka viongozi wa Afrika Magharibi kufikiria "kuondoa vikwazo vyote vilivyowekwa dhidi ya Burkina Faso, Guinea, Mali na Niger."

Pia ametoa wito kwa Burkina Faso, Mali na Niger kufikiria upya uamuzi wao wa kuondoka katika jumuiya hiyo. "Tafadhali, tafadhali sitisheni uamuzi wenu, rudieni," aeongeza. Nchi hizo tatu ni wanachama waanzilishi wa ECOWAS iliyoundwa mwaka 1975, lakini ilizisimamisha kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyopindua serikali zilizochaguliwa za kiraia. ECOWAS iliweka vikwazo vizito vya kiuchumi na kifedha dhidi ya Mali na Niger, ambavyo bado vinatumika dhidi ya utawala wa kijeshi wa Niger.

Siku ya Jumatatu, jeshi la Guinea, ambalo lilichukua mamlaka kwa mapinduzi mnamo Septemba 2021, liliamuru kuvunjwa kwa serikali.

Bw. Gowon alitawala Nigeria kuanzia mwaka 1966 hadi 1975, huku vita vya wenyewe kwa wenyewe vikiendelea kusini-mashariki mwa nchi hiyo kufuatia kutangazwa kwa uhuru wa Jamhuri ya Biafra na Waigbo waliojitenga mwaka 1967. Vita, Njaa na magonjwa vimesababisha vifo vya zaidi ya milioni moja katika kipindi hiki. Jenerali Yakubu Gowon, ambaye sasa ana umri wa miaka 89, alimtembelea rais wa sasa wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu, Jumatano kabla ya kutoa hotuba yake, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Rais wa Tume ya ECOWAS, Omar Alieu Touray, amesema Bw. Gowon ametoa "ujumbe wa nguvu". Bw. Touray, ambaye alithibitisha kufanyika kwa mkutano wa kilele usio a kawaida wa ECOWAS siku ya Jumamosi, amemwambia Bw. Gowon kwamba "viongozi watazingatia ujumbe wako wakati wa majadiliano yao."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.