Pata taarifa kuu

Anga ya Niger yafungwa kwa safari za ndege kutoka na kwenda Nigeria

Hati kutoka kwa Shirika la Usalama wa Usafiri wa Anga barani Afrika na Madagascar (Asecna) ya tarehe 7 Februari na kuchapishwa kwenye mtandao, inathibitisha kufungwa kwa anga ya Niger kwa safari za ndege kutoka na kwenda Nigeria.

Abiria wanapanda ndege nchini Nigeria, Julai 9, 2020.
Abiria wanapanda ndege nchini Nigeria, Julai 9, 2020. AP Photo/Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Shirika la Usalama wa Urambazaji (Asecna), la tarehe 7 Februari, kwa hakika imebainisha kwamba "anga ya Jamhuri ya Niger iko wazi kwa safari zote za ndege za kibiashara, kimataifa na kitaifa, isipokuwa kwa ndege za kibiashara kwenda au kutoka Nigeria [...]. Vizuizi hivi haviathiri safari za ndege za kibiashara zinazoruka juu ya anga ya Nigeria bila kutua huko,” inabainisha hati ya Asecna.

Waziri wa maendeleo wa Ujerumani anaonekana kukabiliwa na vikwazo hivi wiki hii. Siku ya Jumatano Februari 7, ndege yake ilipigwa marufuku kuingia katika anga ya Niger na ilibidi irudi kutua Abuja, kutoka pale ilipopaa. Hatimaye waziri huyo alilazimika kutoingia katika anga ya Niger ili kurejea Ulaya.

Taarifa hii kutoka kwa shirika hili la kikanda linaonekana kujibu taarifa kutoka kwa shirika la Usimamizi wa Anga la Nigeria (NAMA), iliyochapishwa mnamo Januari 29. Hii inaonyesha kwamba "safari zote za ndege za kibiashara" zinazotoka Niger au kwenda Niger, kutoka Nigeria, pamoja na ndege za kibiashara "kutoka Niger na kuruka juu ya anga ya Nigeria" "zimesimamishwa", "kulingana na maazimio ya ECOWAS".

Safari maalum za ndege, safari za ndege katika hali ya hatari na safari za ndege zinazopitia anga ya Niger haziahusiki na hatua hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.