Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-USALAMA

Vijana wawili wauawa, Senegal yatumbukia katika mgogoro

Senegal, inayotikiswa kwa siku kadhaa na uamuzi tata wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais, imetumbukia katika mgogoro mkubwa siku ya Jumamosi baada ya kukandamizwa kwa maandamano ambapo vijana wawili waliuawa.

Siku ya Jumamosi, askari wa jeshi la Senegal walishika doria katika mitaa ya Dakar baada ya makabiliano siku moja kabla ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais uliopingwa na upinzani na mashirika ya kiraia.
Siku ya Jumamosi, askari wa jeshi la Senegal walishika doria katika mitaa ya Dakar baada ya makabiliano siku moja kabla ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais uliopingwa na upinzani na mashirika ya kiraia. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Ukandamizaji huo ulizua wimbi la hasira miongoni mwa upinzani. "Tunatoa wito kwa jumuiya ya kikanda na kimataifa kuwa mashahidi kutokana na hali kupindukia kwa mamlaka haya yasiyofaa" ya Rais Macky Sall, amesema Khalifa Sall, mmoja wa wagombea wakuu wa urais. Thierno Alassane Sall, mgombea mwingine, alipinga kwenye mtandao wa X dhidi ya "ukandamizaji wa kikatili usiokubalika".

Nchi imeguswa na kuhuzunishwa na kifo cha Alpha Yoro Tounkara, 22, mwanafunzi wa mwaka wa pili katika kitivo cha jiografia kilichotokea katika mji wa kihistoria wa Saint-Louis (kaskazini). Mamia ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Gaston Berger, alikokuwa akikosomea, walikesha usiku kucha kuanzia Ijumaa kuamkia Jumamosi, wakimwombea.

"Hakuwa tu mwanafunzi mahiri, bali pia mwenzetu anayependwa na kuheshimiwa. Uwepo wake na ucheshi wake kwa kila mtu utakosekana kwa wale wote waliobahatika kumfahamu," ameandika Cheikh Ahmadou Bamba Diouf, rais wa klabu ya jiografia katika Chuo Kikuu cha Gaston Berger.

Mazingira ya kifo chake bado hayajajulikana lakini uchunguzi umefunguliwa, amesema mwendesha mashtaka wa umma wa Saint-Louis. Waziri wa Mambo ya Ndani amebainisha katika taarifa yake "kwamba vikosi vya ulinzi na usalama havikuingilia kati katika chuo kikuu ambapo kifo kilitokea."

Amepigwa risasi

Modou Gueye, 23, ni mwathirika wa pili wa maandamano hayo. Alikuwa mchuuzi wa mitaani huko Colobane, eneo lenye shughuli nyingi mjini Dakar, ambapo alikuwa akiuza jezi na bendera. "Kulikuwa na mabomu ya machozi yaliyorushwa, na kisha tukaenda kituo cha basi za mwendo kasi huko Colobane  ili tuweze kurudi nyumbani," kaka yake, Dame Gueye, ameliambia shirika la habari la AFP. "Hapo ndipo afisa wa polisi alimpiga risasi moja kwa moja tumboni," amesema. "Mimi ndiye niliyeshikilia begi lake alipoanguka," ameongeza.

"Alifanyiwa upasuaji mara mbili jana usiku na kwa bahati mbaya, alifariki dunia asubuhi ya leo," Mbagnick Ndiaye, shemeji yake, aliliambia shirika la habari la AFP. Habari hiyo haijathibitishwa na mamlaka. Picha zilizoruhwa kwenye mitandao ya kijamii huongeza hofu ya majeraha mengi katikaukandamizaji uo wa polisi.

Siku ya Ijumaa, maandamano makubwa ya kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi na Rais Macky Sall yalifanyika nchini kote, hasa huko Dakar, lakini yakatawanywa mara moja na vikosi vya usalama. Katika mji mkuu, polisi walitumia vitoa machozi kwa wingi kuwazuia watu waliokuwa wakijaribu kukusanyika eneo la Place de la Nation.

Waandamanaji walijibu kwa kurusha mawe na kuweka vizuizi barabarani. Wito wa kuandamana siku ya Ijumaa ulitangazwa kwenye mitandao ya kijamii, bila kuwezekana kubaini ni nani alitoa wito huo. Maandamano hayo kwa ujumla yamepigwa marufuku nchini humo.

Waandishi Wasio na Mipaka (RSF) "wamekasirishwa" na kulengwa kwa angalau waandishi watano, huku wakinyooshea polisi kidole cha lawama huko Dakar.

Senegal imekuwa ikikumbwa mara kwa mara tangu 2021 na matukio ya maandamano yanayohusishwa na kesi za kisheria dhidi ya mmoja wa wapinzani wakuu, Ousmane Sonko, ambaye sasa yuko jela, huku makumi ya watu wakiuawa na mamia kukamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.