Pata taarifa kuu

Wahusika wa uhalifu hawaadhibiwi, zaidi ya miaka 20 baada ya kuanza kwa vita Darfur

Zaidi ya miaka 20 iliyopita, vita vilianza huko Darfur, vikigubikwa na ukatili. Leo, Sudan ya magharibi imeingia tena katika hali ya kutisha na ulimwengu, wakaazi na wataalam wanashutumu, kwa mara nyingine tena utawala ambao hauwaadhib wahalifu wa vitendo hivyo vya kikatili.

Vita hivyo kwa mara nyingine tena vimeleta unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa kikabila.
Vita hivyo kwa mara nyingine tena vimeleta unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa kikabila. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Kizazi, kilicholelewa katika kambi za watu waliokimbia makazi yao, kilitupwa barabarani tena wakati mzozo kati ya jeshi, linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), kinachoongozwa na Jenerali Mohammed Hamdane Daglo, ulianza mwezi wa Aprili 2023.

Vita hivi kwa mara nyingine tena vimeleta unyanyasaji wa kijinsia, unyanyasaji wa kikabila na matukio ya maeneo kuchomwa moto. Kulingana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa, katika mji wa El-Geneina pekee, huko Darfur Magharibi, kati ya watu 10,000 na 15,000 waliuawa, au 5% ya wakazi.

Kulingana na wataalamu hao, mashambulizi "yalipangwa, yaliratibiwa na kutekelezwa na RSF na wanamgambo washirika wa Kiarabu", ambao "walilenga kwa makusudi vitongoji vya raia (...), kambi za watu waliokimbia makazi yao, shule, misikiti na hospitali, pia kupora nyumba na maeneo ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa na Umoja wa Mataifa".

"Walilenga kwa makusudi Massalit", kabila kubwa lisilo la Waarabu katika jiji hilo, wanaongeza, wakizingatia uwezekano wa "uhalifu wa kivita au uhalifu dhidi ya binadamu" huko Darfur, ukubwa wa Ufaransa ambapo robo ya Wasudani milioni 48 wanaishi.

Majenerali "makatili na wahalifu"

Leo hii, RSF inashikilia miji mikuu minne kati ya mitano ya Darfur na, anasema mtafiti aliyeko nje ya Sudan ambaye anazungumza kwa sharti la kutotajwa jina, "majambazi ambao wamewatisha watu kwa miongo kadhaa wanatawala: wanabaka, kupora, wanaua watu wengi kulingana na kabila.

Huko Zalingei, mji mkuu wa Darfur ya Kati, mnamo Oktoba 31, watu wa Four, kabila ambalo Darfur lilichukua jina lake, waliteswa "kama walivyoteswa Wamassalit huko El-Geneina", mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la haki za binadamu la Awafy, mwenyewe mkimbizi nje ya nchi, Mohamed Bera, ameliambia shirika la habari la AFP.

Siku hiyo, RSF ilichukua jiji hilo kwa gharama ya "mauaji ya watu wengi, mauaji ya kikatili, watu kufungwa kiholela, unyanyasaji wa kijinsia, mateso na uporaji," anashutumu. Tangu mwezi Mei,  mawasiliano ya simu yanafanya kazi kwa shida huko Darfur.

Wanachama wa Awafy walihesabu "angalau watu 180 waliouawa" katika shambulio kwenye kambi ya watu waliotoroka makaazi yao ya Hassaheissa ambapo RSF ilihakikisha kwamba "jeshi lilipata kimbilio". Kote Darfur, "wengi wa watu milioni tatu ambao tayari wamehama" wameendelea kukimbia "kwa mara ya pili au ya tatu", wanaongeza. Kiongozi wa kabila anaihakikishia AFP kwamba angalau kambi nne za watu waliokimbia makazi yao huko Darfur Magharibi "zimechomwa moto".

Mwaka 2003, Janjawids - wanamgambo wa Kiarabu ambao tangu wakati huo waliingizwa katika RSF - waliongoza sera ya amauaji kwa niaba ya rais Omar al-Bashir na jeshi lake. Mwaka uliofuata, Marekani ilizingatia kwamba ukatili uliofanywa huko Darfur ulifikia ufafanuzi wa "mauaji ya halaiki".

Leo, wakazei wa Darfur wanakabiliwa na mapigano ya RSF na jeshi. Na, anabainisha mtafiti Alex de Waal, Jenerali Burhane "si mkatili" kama makamu wake wa zamani Daglo. "Siyo tu" jeshi halikuwalinda raia, lakini pia "lilitekeleza mashambulizi (...) katika maeneo ya mijini" kama El-Facher, El-Daein na hasa Nyala, wanasema wataalam wa Umoja wa Mataifa.

"Sio mkakati"

Mwezi Desemba, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alishutumu jeshi na RSF kwa "uhalifu wa kivita (...) uhalifu dhidi ya binadamu na vitendo vya maangamizi ya kikabila".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.