Pata taarifa kuu

Nigeria: Mji wa Mangu wakumbwa na mshtuko kutokana na ghasia

Eneo la Kaskazini-kati mwa Nigeria, mji mdogo wa kilimo wa Mangu, ambapo Waislamu na Wakristo wameishi pamoja kwa muda mrefu, umeingia kwenye ghasia ambazo hivi karibuni zilisababisha dazeni kadhaa za vifo.

Kwa miaka mingi, mji wa Mangu umeepuka ghasia kati ya jamiia zinazozuka mara kwa mara katika Jimbo la Plateau.
Kwa miaka mingi, mji wa Mangu umeepuka ghasia kati ya jamiia zinazozuka mara kwa mara katika Jimbo la Plateau. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Kuta za manjano zilizoungua za msikiti mkubwa wa kati wa Mangu ambao mbele yake ardhi imetapakaa na vifusi, sawa na kanisa lililoteketezwa kabisa la Cocin Kwhagas, kilomita chache kutoka hapo, zinaonyesha kwamba hakuna hata jamii hizi mbili za kidini ambazo zimepukana na hali hiyo.

Kwa miaka mingi, mji wa Mangu umeepuka ghasia kati ya jamii zinazozuka mara kwa mara katika Jimbo la Plateau. Jimbo hili, lililo kwenye mstari unaogawa kaskazini mwa Nigeria, eneo ambalo lina Waislamu wengi, na kusini, eneo ambalo lina Wakristo wengi, ni kitovu cha vurugu kati ya jamii hizi.

Wakitokea katika kabila la Mwaghavul, Waislamu na Wakristo kutoka Mangu wamekuwa wakiishi pamoja. Lakini mwishoni mwa mwezi wa Januari 2024, jiji hilo lililengwa na mashambulizi kadhaa yaliyotekelezwa kwa kutummia bunduki na mapanga. Makanisa, misikiti na shule zilichomwa moto kwa makusudi, wakaazi na Shirika la Msalaba Mwekundu wamesema.

Takriban watu 25 waliuawa hapo kati ya Januari 22 na 23, wakati huo huo shambulizi lingine katika kijiji jirani chenye Wakristo wengi lilisababisha watu 30 kuuawa. Ghasia hizo zilikuja wiki kadhaa baada ya msururu wa mashambulizi katika kipindi cha Krismasi ambapo karibu watu 200 waliuawa katika maeneo  jirani ya Bokkos na Barkin Ladi, katika Jimbo la Plateau.

Huko Mangu, mamlaka bado haijawabaini watu waliohusika na mashambulizi hayo, na hivyo kutoa nfasi ka uvumi. Kwa baadhi, jiji hilo lilishambuliwa na majambazi, wakati wengine wabaini kwamba ilikuwa vurugu kati ya jamii hizi mbili.

“Salama zaidi”

Mbele ya magofu ya nyumba ya familia yake iliyoteketezwa, mkazi wa Mangu, Jabira Rabio, anasema kundi la watu lilishambulia mtaa wake nje kidogo ya jiji na kufyatua risasi kabla ya kuchoma moto nyumba. "Tulikimbia tukiwa na nguo tu migongoni. Mali yangu yote ndani ya nyumba yangu iliungua," amesema muuzaji huyo wa mifugo.

Kuta za waridi zilizoungua za nyumba yake sasa zimezungukwa na majivu. Ndani, kilichobaki ni sahani chache zilizovunjika, mavazi ya harusi ya mtoto wake yaliyowaka moto na zulia lililochomwa. "Hatuwezi kusema kilichotokea. Ilitokea ghafla. Tumeishi pamoja kwa amani," anasema.

Mita chache kutoka kanisa la Cocin Kwhagas huko Mangu, makumi ya nyumba za Wakristo zilichomwa moto, kulingana na wakaazi. "Wakristo wengi katika mtaa wangu (Lahir) wameondoka na kwenda kuishi kwingine. Ninahisi salama zaidi hapa ambako kuna Wakristo wengi zaidi," anaeleza Gideon Timothy, 33, mtayarishaji wa muziki.

"Tuliomba na kuomba"

Kulingana na ripoti ya shirika la Msalaba Mwekundu ambayo shirika la habari la AFP lilipata kody, zaidi ya watu 8,000 wameyakimbia makazi yao kutokana na ghasia huko Mangu na viunga vyake. Wengi wao wamepata kimbilio katika maeneo mengine ya jiji ili kukaa karibu na familia zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.