Pata taarifa kuu

Sudan: Wasiwasi watanda juu ya kuenea kwa silaha na kuongezeka kwa vita

Nchini Sudan, tangu Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF) walipoteka jimbo la al-Jazirah, wito wa kuwapa silaha raia katika majimbo mengine umeongezeka.

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa majeshi ya Sudan, akiwasili katika uwanja wa ndege wa kijeshi katika mji wa Port Sudan, Agosti 27, 2023.
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa majeshi ya Sudan, akiwasili katika uwanja wa ndege wa kijeshi katika mji wa Port Sudan, Agosti 27, 2023. REUTERS - IBRAHIM MOHAMMED ISHAK
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu, Januari 8, gavana wa al-Kadarif, jimbo lililoko mashariki mwa nchi, alitoa wito kwa wakazi wa Kadarif kuchukua silaha katika kukabiliana na kusonga mbele kwa wanamgambo wa RSF. Pande mbili zinazopigana, jeshi na wanamgambo ambao wamekuwa wakipingana na kuwania madaraka tangu Aprili 15, wanasajili wapiganaji wapya kwa kasi ndefu.

Baada ya kuteka sehemu kubwa ya jimbo la al-Jazirah, wanamgambo wa FSR wa Jenerali Mohamad Hamdane Daglo wanaendelea na mafanikio yao na kuahidi kuyateka majimbo mengine jirani, Kusini, Kaskazini na Mashariki mwa nchi. Katika kila kijiji, kikosi hiki kinawataka wakazi kutoa "vijana wao" ili "kulinda eneo lao". Wanawapa magari 4x4 na bunduki aina ya Kalashnikov. Vijana hawa kwa kweli wameorodheshwa katika safu ya FSR.

Hofu ya silaha kuenea nchi nzima

Kwa upande wa jeshi la Sudan, lilianzisha kampeni kubwa: upinzani wa watu wenye silaha katika Nile Nyeupe, huko Kadarif, Kaskazini, Kassala na Bahari ya Shamu. Magavana wa majimbo haya wanatangaza kwamba wanataka kuwafunza vijana kubeba silaha na kuwatia moyo wajihusishe ili "waweze kutetea ardhi zao, heshima yao na familia zao". Huko Soaken, katika Bahari Nyekundu, kiongozi wa makabila ya el-Baja pia anashinikiza kujilinda.

Mashindano haya ya silaha kati ya raia yanazua hofu ya kusambaa kwa silaha kwa kiasi kikubwa nchini. Vyama vya kiraia na hasa muungano wa Forces for Freedom and Change vinaongeza maonyo dhidi ya kuenea kwa silaha na kutoa wito kwa wananchi kutofuata kampeni hizi mbaya zinazoweza kuendeleza vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.