Pata taarifa kuu
VITA-USALAMA

Sudan: Jenerali Al-Burhan apaza sautibaada ya kuanguka kwa mji wa Wad Madani

Mji wa Wad Madani, mji mkuu wa jimbo la Al-Jazirah, ulitekwa na wanamgambo wa FSR (Rapid Support Forces) siku ya Jumatatu. Pigo kwa jeshi la Sudan kwa kupoteza mji huona maafa mapya ya kibinadamu. Jenerali al-Burhan alikosolewa vikali siku ya Alhamisi Desemba 22, baada ya jeshi kupoteza mji huo. Jenerali al-Burhan ametaka kuonyesha msimamo wake ulio thabiti.

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, wakati wa mkutano huko Saudi Arabia, Novemba 11, 2023.
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, wakati wa mkutano huko Saudi Arabia, Novemba 11, 2023. © AFP PHOTO / HO/ SAUDI PRESS AGENCY
Matangazo ya kibiashara

Kwa hotuba yake ya kwanza tangu kuanguka kwa mji wa Wad Madani, Jenerali al-Burhan ametaka kuonyesha kwamba bado yuko imara na amejizatiti vilivyo. Mkuu wa jeshi amesisitiza tena kwamba wanajeshi wake bado wanaonyesha umoja na wanashikamana kwa kilinda nchi. Hata hivyo ameahidi kuwa atawajibisha askari walioamua kurudi nyuma na kuacha kupambana na adui. Uchunguzi ambao haujawahi kushuhudiwa pia umefunguliwa kufuatia kukataa kutii amri ya kupambana na adui.

Inapaswa kusemwa kwamba tangu Jumatatu, mkuu wa jeshi amekuwa dhaifu. Mara kadhaa, viongozi wa kisiasa wamelishutumu jeshi hilo kwa kuwahadaa watu au kwa kufuata mkakati mbaya. Maoni haya yanasaliti hisia za watu kuachwa na hasira dhidi ya jeshi ambalo liliahidi kuwalinda. Baada ya siku nne za mapigano katika vitongoji vya mji huo, RSF iliingia kwa urahisi Wad Madani, wakati jeshi lilikuwa tayari limeondoka katika mji huo.

Hofu ya kuporomoka kwa mfumo wa afya wa Sudan

Siku ya Alhamisi, chama cha madaktari kilisema wanajeshi tayari walikuwa wakipora na kuharibu vituo vya afya. Kulingana na chama hicho, hospitali 22 za jiji hilo sasa hazifanyi kazi. "Wad Madani imekuwa kituo kikuu tangu 90% ya hospitali za Khartoum kuamua kufunga milango. Hii inasababisha kuporomoka kabisa na hatari kwa mfumo wa afya,” chama cha madaktari kilisema.

Kwa kuchukua udhibiti wa jiji hili, RSF sasa itaweza kutembea kwa uhuru katika Jimbo lote la Al-Jazeera na kufanya mashambulizi kuelekea pande kadhaa, ikiwa ni pamoja na Gedaref, Sennar au Kosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.