Pata taarifa kuu

Nigeria: Rais Tinubu ataka uchunguzi baada ya shambulizi la droni kuwaua watu 85

Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ameagiza kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu shambulio la mwishoni mwa juma lililofanywa na jeshi la nchi hiyo, ambapo watu 85 waliuawa, wakiwemo wanawake na watoto kaskazini mwa mji wa Kaduna.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu
Rais wa Nigeria Bola Tinubu AP - Lewis Joly
Matangazo ya kibiashara

Raia hao walikuwa wakihudhuria sherehe ya kiislamu kwenye mji wa Tudun-Biri, tukio lililoamsha hasira za raia wa Nigeria.

Tukio hili lilisababisha jeshi kulazimika kutoa taarifa kwa umma kueleza kilichotokea, ambapo kupitia kwa kamishna wa polisi kwenye enei la Kaduna, Samuel Aruwan, alikiri jeshi kufanya makosa.

Jeshi la Nigeria limeeleza mazingira ya tukio lilivyokuwa ya shambulio ambalo halikukusudiwa. Jeshi lilikuwa katika misheni ya kawaida dhidi ya magaidi lakini kwa bahati mbaya raia walikuwepo pia na waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini kwa msaada wa serikali. 

Licha ya jeshi kutotoa taarifa rasmi za majeruhi, mashuhuda wanasema mamia ya watu walijeruhiwa, wakieleza namna mlipuko wa kwanza ulivyotokea kabla ya kufuatiwa na mingine, Ashiru Ibrahim ni miongoni mwao.

Nilikuwa nyumbani niliposkia mlio na mimi nikatoka nje haraka nikaona mlipuko na miili ya watu kwa kweli ilikuwa imetapakaa. Hata kabla ya kufika hospitali tukaskia tena mlipuko mwingine.

Awa Yakubu, nae kutoka kijiji hikohiko alishuhudia kilichotokea siku ya Jumapili.

Tulikuwa na sherehe ya maulid, wakati tuliposkia mlio wa sauti ya ndege ya kivita na kabla hatujamaliza kushangaa, bomu lilirushwa, watu wengi walikufa. Tulijeruhiwa lakini tulifanikiwa kukimbia na baadhi ya vijana walijaribu kuwaokoa wengine lakini kwa bahati mbaya na wao waliuawa katika mlipuko wa pili.

Kwa muda sasa jeshi la Nigeria, limekuwa likitumia ndege zisizo na rubani kushambulia ngome za wanajihadi wa kiislamu wa kundi la Boko Haram kaskazini mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.