Pata taarifa kuu
MARIDHIANO-SIASA

Chad: Mwanasiasa wa upinzani Succès Masra arejea baada ya mwaka akiwa uhamishoni

Nchini Chad, mwanasiasa wa upinzani Succès Masra amewasili saa sita mchana, saa za Chad, kwenye uwanja wa ndege wa Ndjamena. Kiongozi huyo wa chama cha Les Transformateurs amepokelewa kwenye uwanja wa ndege na mawaziri wa Maridhiano ya Kitaifa, Abderaman Koulamallah, na wa Mawasiliano, Aziz Mahamat Saleh.

Mwanasiasa wa upinzani Succès Masra aliporejea Ndjamena baada ya mwaka mmoja akiwa uhamishoni, Novemba 3, 2023.
Mwanasiasa wa upinzani Succès Masra aliporejea Ndjamena baada ya mwaka mmoja akiwa uhamishoni, Novemba 3, 2023. © Carol Valade/RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Ndjamena, Carol Valade

Succès Masra alikuwa amevaa suti ya bluu, tai nyekundu na miwani ya jua. Alipitia lango la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hassan Djamous saa 12:30 mchana kwa saa za Chad mnamo Novemba 3, 2023, akipokelewa na Mawaziri wa Maridhiano na Mawasiliano ya Kitaifa, kabla ya kuingia katika gari jeusi hukuakishusha kioo cha dirisha la gari kwa muda mfupi ili kuwasalimia waandishi wa habari adimu waliokuwepo. Kwa sababu ujio huu ulifanyika kwa siri kubwa.

Ujumbe huo mara moja ulielekea Wizara ya Maridhiano ambapo Succès Masra alizungumza maneno machache kwenye microfone ya RFI. "Hakuna kitu bora kuliko kwenda nyumbani," amesema kabla ya kutangaza "siku 40 za maombolezo, kutafakari, kusikiliza na mshikamano (...) kwa minajili ya kuponya majeraha na kusonga mbele".

Majadiliano yamekuwa yakiendelea kati ya Succès Masra na serikali chini ya uongozi wa mwezeshaji katika mgogoro wa Chad, Rais wa DRC, Félix Tshisekedi. Makubaliano yalitangazwa mjini Kinshasa mnamo Oktoba 31.

Succès Masra aliondoka nchini siku moja baada ya ukandamizaji wa umwagaji damu wa maandamano mnamo Oktoba 20, 2022. Hati ya kimataifa ya kukamatwa ilitolewa dhidi yake. Kurudi kwake kumewezeshwa na kutiwa saini kwa makubaliano na serikali, kufuatia upatanishi huko Kinshasa mnamo Oktoba 31, 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.