Pata taarifa kuu

Kura ya maoni ya Katiba nchini Chad: miungano ya kisiasa yazindua shughuli zao za kampeni

Kampeni ya kura ya maoni imeanza Jumamosi Novemba 25 nchini Chad. Wananchi wa Chad wanaitwa kupiga kura mnamo Desemba 17 ili kuwezesha kurejea kwa utaratibu wa kikatiba kwa kupiga kura "Ndio" au "Hapana" kwa sheria mpya ya kimsingi ambayo inadumisha muundo wa umoja wa taifa. Miungano ya vyama vya kisiasa kwa kambi za "ndio" na "hapana" imezindua rasmi shughuli zao za kampeni siku ya Jumamosi huko Ndjamena.

Kituo cha kupigia kura nchini Chad.
Kituo cha kupigia kura nchini Chad. AFP PHOTO / Gael COGNE
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Ndjamena, Olivier Monodji

Kampeni hii ya siku ishirini itawezesha mielekeo tofauti ya kisiasa kujadiliana na watu kuhusu uchaguzi wa aina ya taifa.

Mchakato ambao unabadilisha kadi za mchezo wa kisiasa: baadhi ya vyama vya siasa vilivyompinga Rais wa zamani Idriss Déby, leo vinamuunga mkono mwanawe, Mahamat Idriss Deby. Hiki ndicho kisa cha mpinzani wa zamani wa kihistoria, Saleh Kebzabo, Waziri Mkuu wa sasa wa mpito. Yeye ndiye rais wa muungano huu kwa kupendelea "Ndiyo" kwa Katiba mpya.

"Imani yetu katika serikali ya umoja, iliyogawanyika sana, ambapo haki na usawa vitakuwa dira ya utawala bora. Katiba hii mpya, ambayo tunakuomba upige kura kwa wingi, inajumuisha watu wote. "

Kwa upande wake, muungano unatotetea kura ya "Hapana" , muungano wa vyama vinavyopendelea serikali ya shirikisho, una wasiwasi kuhusu udanganyifu unaoweza kutokea siku ya kupiga kura.

“Ninaamini kwamba mamlaka za serikali, zilizoshiriki katika kampeni ya ‘Ndiyo’, zinafanya makosa ya kisiasa. Na tunajua, kwa hakika, kwamba kura ya 'Hapana' itashinda. Sasa, lazima tuzuie udanganyifu," amesema Brice Mbaimon Guedmbaye, msemaji wa muungano wa vyama vinavyotetea kura ya "Hapana".

Wakati huo huo, mashirika ya kiraia yamewasilisha ombi kwa mamlaka ya mahakama kuomba kusimamishwa kwa muungano huu wa "Ndio" katika kura ya maoni ya katiba. Kulingana na wao, uwepo wa mkuu wake kama Waziri Mkuu wa mpito utakiuka kanuni ya kutoegemea upande wowote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.