Pata taarifa kuu

Nigeria: Mahakama ya Juu yaidhinisha ushindi wa Rais Tinubu

Mahakama ya Juu nchini Nigeria, imetupilia mbali kesi iliyokuwa imawasilishwa na waliokuwa wagombea wakuu wawili wa upinzani, waliotaka ushindi wa rais Bola Ahmed Tinubu kufutwa kwa madai kuwa uchaguzi wa mwezi Februari haukuwa huru na haki.

Bola Tinubu, Rais wa Nigeria, akiwasili kwa ajili ya kuhitimisha Mkutano wa New Global Financial Pact Summit, Ijumaa, Juni 23, 2023 mjini Paris, Ufaransa.
Bola Tinubu, Rais wa Nigeria, akiwasili kwa ajili ya kuhitimisha Mkutano wa New Global Financial Pact Summit, Ijumaa, Juni 23, 2023 mjini Paris, Ufaransa. © Lewis Joly/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umetolewa na Majaji saba, wa Mahakama hiyo, ambao unamaanisha ushindi wa Tinubu ni halali.

 

Waliokuwa wagombea wawili wa urais, Atiku Abubakar na  Peter Obi, waliwalisha kesi, wakidai kuwa Tinubu aliiba kura, na sheria za uchaguzi zilikiukwa wakati wa uchaguzi huo kumpendelea mpinzani wao.

Aidha, wapinzani hao walitaka Mahakama kubaini kuwa, cheti cha Tinubu kutoka chuo kikuu cha Chicago nchini Marekani, alichotumia kuomba nafasi ya kugombea urais, hakikuwa halali.

Jaji John Inyang Okoro akisoma uamuzi huo, alisema baada ya kusikiliza kesi hiyo kutoka kwa wapinzani, hakukuwa na ushahidi kubadilisha ushindi wa Tinubu.

Kesi hiyo ilifka kwenye Mahakama hiyo ya juu, baada ya Mahakama ya rufaa kutupilia mbali shauri hilo, ambalo pia lilitupiliwa mbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.