Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Rais anayemaliza muda wake Sissi kuwania muhula wa 3

Abdel Fattah al-Sissi, akiwa madarakani nchini Misri tangu alipompindua Mohamed Morsi mnamo 2013, ametangaza Jumatatu jioni nia yake ya kuwania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi wa rais mnamo mwezi wa Disemba, uchaguzi katikati ya mzozo wa kiuchumi ambao unaonekana kuwa ngumu zaidi kuliko zile zilizopita.

Abdel Fattah al-Sissi anatangaza nia yake ya kuwania kwenye kiti cha urais kwa mara ya tatu na ya mwisho kulingana na Katiba ambayo alibadilisha ili kuweza kuwania katika uchaguzi huo.
Abdel Fattah al-Sissi anatangaza nia yake ya kuwania kwenye kiti cha urais kwa mara ya tatu na ya mwisho kulingana na Katiba ambayo alibadilisha ili kuweza kuwania katika uchaguzi huo. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mkutano huo wakati ambapo alifanyika "miaka kumi ya kufaulu", kiongozi huyo wa Misri amesema anataka "kuwania ili kuendelea na shughuli mbaimbali kwa muhula huu mpya". Ninawaalika "wapiga kura wote kupiga kura, hata ikiwa hawatanipigia mimi kura," ameongeza.

"Sote tuliingia barabarani kumuunga mkono rais Abdel Fattah al-Sissi kwa miradi yake mikubwa, hakuna mtu bora kama yeye kwa siku zijazo," mmoja wa wafuasi wake, Hassan Afifi, mwalimu aliyekuja na wanafunzi wake katika moja ya maeno huko Cairo ameliamia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.