Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Misri: Uchaguzi wa urais Kufanyika kuanzia Desemba 10 hadi 12, 2023

Mamlaka ya kitaifa ya Uchaguzi ya Misri imetangaza siku ya Jumatatu tarehe za uchaguzi ujao. Kwa hivyo duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais wa Misri itafanyika kuanzia tarehe 10 hadi 12 Desemba.

Mwanamke akipiga kura katika kituo cha kupigia kura huko Esna, kusini mwa mji wa kusini mwa Misri wa Luxor, Oktoba 24, 2020, wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge.
Mwanamke akipiga kura katika kituo cha kupigia kura huko Esna, kusini mwa mji wa kusini mwa Misri wa Luxor, Oktoba 24, 2020, wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge. AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Cairo, Léonie Lebrun

Ni wakati wa kongamano lenye mvuto mkubwa ambapo mamlaka ya kitaifa ya uchaguzi imezindua kalenda yake uchaguzi kwa mamia ya wanahabari. Kampeni za uchaguzi wa urais zitaanza Novemba 8, kabla ya duru ya kwanza kutoka Desemba 10 hadi 12.

Kwa uchaguzi huu, mamlaka ya uchaguzi inatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi. "Mjieleze kwenye uchaguzi na muamue hatima yenu ambayo iko mikononi mwaenu, muwe kielelezo kwa watu kama ulimwengu unavyozoea kutuona," mkuu wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Walid Hassan Hamza amesema. Matokeo ya duru ya kwanza yatatangazwa Desemba 18.

Kwa waangalizi wengi, wapinzani na wananchi, wanaona kuwa matokeo ya kura hiyo yanatia shaka kidogo kutokana na rais Sissi aliyepo kila mahali kung'ang'ania madarakani ambaye hata kupitia kura ya maoni alipata kuongezwa muda wa mamlaka yake ya sasa na haki ya kuwania muhula wa tatu. Wengi wa Wamisri pia hawaamini kuwa kutakuwepo na duru ya pili na tayari wanafikiria muhula mpya wa Rais Sissi. Lakini mkuu wa nchi hajatangaza rasmi kuwania kwenye kiti cha urais.

Kwa vyovyote vile, mamlaka ya kitaifa ya uchaguzi imewaonya watu wenye nia mbaya ya kuchochea vurugu. "Mjiepusheni na uvumi na uongo, zuieni njama zinazopangwa na watu wenye chuki na mfahamu kwamba njia pekee ya kudhoofisha hatua ya Mamlaka ya taifa ya uchaguzi ni kujaribu kuwatia hofu na mashaka mioyoni mwenu," Mkuu huyo wa Tume amesema.

Ikiwa kutakuwa na duru ya pili, itafanyika kuanzia Januari 8 hadi 10. Na matokeo ya mwisho yatatangazwa Januari 16.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.