Pata taarifa kuu

Ghana: Upinzani unamtaka gavana wa benki kuu kujiuzulu

Chama kikuu cha upinzani nchini Ghana, kimetoa makataa ya wiki tatu kwa gavana wa benki na naibu wake kujiuuzulu.

Upinzani nchini Ghana umemtaka gavana wa benki kuu na naibu wake kujiuuzulu
Upinzani nchini Ghana umemtaka gavana wa benki kuu na naibu wake kujiuuzulu © Bank of Ghana
Matangazo ya kibiashara

The National Democratic Congress kinamtuhumu Ernest Addison mkuu wa benki hiyo kwa uongozi mbaya, benki hiyo ikikashifiwa kwa kuchapisha pesa kinyume na sheria pamoja na kutumia zaidi ya dolla milioni 8.6 kwa gharama za usafiri.

Ripoti ya hivi punde ya kila mwaka ya benki kuu imeonyesha kwamba ilisajili hasara ya dolla bilioni 5.4 mwaka uliopita.

Benki hiyo tayari imekana tuhumu za chama hicho cha upinzani na kuhusisha hasara hiyo na mpango wa kufanya upya ulipaji wa deni lake kwa mujibu wa makubaliano kati yake na shirika la fedha duniani.

Ghana kwa sasa inajaribu kujiondoa kutoka katika mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi. Mnamo Mei nchi hiyo  ilipata mkopo wa $3bn kutoka kwa IMF kushughulikia mzozo wa kiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.