Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Nigeria: Amri ya kutotoka nje yatangazwa katika Jimbo la Kano

Mahakama ya Nigeria ilibatilisha ushindi wa upinzani katika uchaguzi wa ugavana wa Kano, ambapo chama cha upinzani New Nigeria People's Party (NNPP) kimeshinda dhidi ya All Progressive Congress (APC) chama cha rais Bola Tinubu. Amri ya kutotoka nje ya saa 24 imetangazwa mara moja katika jimbo hili muhimu.

Moja ya maeneo ya mji wa Kano, Nigeria.
Moja ya maeneo ya mji wa Kano, Nigeria. AFP - PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Nchini Nigeria, amri ya kutotoka nje iilitangazwa Septemba 20, 2023 huko Kano, jimbo la pili kwa idadi kubwa ya watu nchini. Hii inafuatia kubatilishwa kwa ushindi wa mgombeawa upinzani katika uchaguzi wa ugavana wa mwezi Machi.

Mahakama ilibatilisha ushindi wa Abba Kabar Yusuf wa chama cha upinzani cha New Nigerian People's Party (NNPP) na kumpendelea Nasuru Yusuf Gawuna wa All Progressives Congress (APC), chama tawala.

Gawuna, aliye karibu na rais wa nchi hiyo Bola Tinubu, alikuwa amepinga matokeo ya uchaguzi huu.

Vikosi vya usalama vimewekwa kwa wingi kwenye barabara kuu ili kuzuia watu kuingia mitaani kwa maandamano.

Mnamo Machi, wapiga kura waliidhinisha mpinzani wake, Abba Kabir Yusuf, kumpa zaidi ya kura milioni moja katika jimbo hili ambalo lilikuwa likiongozwa tangu 2015 na Abdullahi Ganduje wa chama tawala cha APC.

Kisha Gawuna alikashifu tuhuma za udanganyifu wakati wa uchaguzi huu. Kwa hiyo ameshinda tu kesi yake.

Haya ni mafanikio mapya kwa APC, baada ya Abdullahi Ganduje, gavana anayemaliza muda wake kukabiliwa na tuhuma za ufisadi. Mnamo mwaka wa 2017, video ilisambaa ikimuonyesha akiingiza pesa kwenye mifuko yake. Ameendelea kukanushakuwa hana hatia.

Uamuzi huu ni habari njema kwa chama tawala nchini Nigeria. Kwa sababu Jimbo la Kano ndilo lenye idadi kubwa ya wapiga kura, baada ya Lagos, kulingana na tume ya uchaguzi. Kwa hivyo inawakilisha suala muhimu la uchaguzi. Iwapo Rais Bola Tinubu atawania muhula wa pili mwaka wa 2027, atahitaji kudhibiti jimbo hili. Nchini Nigeria, magavana pia wana ushawishi mkubwa, kusimamia bajeti kubwa.

Vile vile, chama cha upinzani, NNPP, pia kinataka kudhibiti Kano, kwani hii itaipa nguvu zaidi katika ulingo wa kisiasa wa kitaifa. Kano ndio jimbo pekee kinaloshikilia.

Abba Kabir Yusuf, gavana wa muda mfupi sana wa Kano, tayari amefahamisha kwamba atapinga uamuzi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.