Pata taarifa kuu

Nigeria: Peter Obi, Atiku Abubakar kupinga ushindi wa Tinubu katika mahakama ya upeo

Wagombea wawili wakuu wa upinzani katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Februari, wamewasilisha kesi katika mahakama ya upeo kupinga hatua ya kutupiliwa mbali kwa kesi yao dhidi ya ushindi wa rais Bola Ahmed.

Atiku Abubakar anataka mahakama ya upeo kubatilisha uamuzi huo wa awali kwa misingi kuwa hakufuata sheria kabla ya kuidhinisha ushindi wa rais Tinubu
Atiku Abubakar anataka mahakama ya upeo kubatilisha uamuzi huo wa awali kwa misingi kuwa hakufuata sheria kabla ya kuidhinisha ushindi wa rais Tinubu © AP/Gbemiga Olamikan
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo iliyokuwa imewasilishwa na Peter Obi wa chama cha Leba na mwenzake Atiku Abubakar wa chama cha PDP ilitupiliwa mbali mwezi jana kwa misingi kuwa hawakuwa na ushahidi wa kutosha kuunga mkono madai yao.

Peter Obi aliyegombea urais kwa tiketi ya chama cha Leba
Peter Obi aliyegombea urais kwa tiketi ya chama cha Leba © Daily Post

Katika uamuzi wao, majaji waliokuwa wanasikiliza kesi hiyo walisema viongozi hao hawakuwa na uwezo wa kutihibitisha kwamba uchaguzi huo wa mwezi Februari ulikuwa na kasoro.

Atiku Abubakar anataka mahakama ya upeo kubatilisha uamuzi huo wa awali kwa misingi kuwa hakufuata sheria kabla ya kuidhinisha ushindi wa rais Tinubu.

Atiku Abubakar aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha  (PDP)
Atiku Abubakar aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha (PDP) AFP

Kwa upande wake Peter Obi anaithumu mahakama kwa kutozingatia masuala ya umuhimu kuhusu madai yake na kesi aliyowasilisha kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu mwa mwezi Februari. Hakuna tarehe iliyotolewa ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.