Pata taarifa kuu

Libya: Jeshi la LNA la Haftar lawasaka na kuwakamata wafuasi wa utawala wa zamani Sirte

Tangu Agosti 15, Jeshi la LNA linaloongozwa na mbabe a kivita Khalifa Haftar limezingira vitongoji kadhaa katika mji wa Sirte, ngome ya kabila la Gaddafi. Kulingana na mashirika kadhaa ya haki za binadamu, lengo muhimu la kutumwa kwa wanajeshi hao ni kuzuia sherehe zilizopangwa kufanyika Septemba 1, kumbukumbu ya mapinduzi yaliyoongozwa na Kanali Muammar Gaddafi dhidi ya Mfalme Senoussi mwaka wa 1969.

Wapiganaji wa kundi la LNA linaloongozwa na Khalifa Haftar Aprili 7, 2019.
Wapiganaji wa kundi la LNA linaloongozwa na Khalifa Haftar Aprili 7, 2019. © REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Takriban raia thelathini wamekamatwa na LNA, kwa sababu ni wakereketwa wa serikali ya zamani na kutaka kusherehekea Septemba 1. Wakati mwingine kwa sababu tu walikuwa na picha za Gaddafi kwenye simu zao. Mdogo wa waliokamatwa ana umri wa miaka 12 tu, mkubwa zaidi ana umri wa miaka 80. Abdallah Issa alipigwa na kutukanwa kabla ya kukamatwa.

Kukamatwa kwa watu hao kulifanywa na kikosi cha Tarek bin Ziad kinachoongozwa na Saddam Haftar. Wanajeshi wa LNA waliwawinda vijana katika mitaa ya Sirte jioni ya Septemba 1. Nyumba zimepekuliwa bila hati ya upekuzi na baadhi ya watu walijikuta nyumba zao zikiharibiwa kwa kuwasha fataki.

Mashirika ya haki za binadamu nchini Libya yameshutumu "kukamatwa kiholela kwa watu hao bila misingi ya sheria". Baraza la Kijamii la kabila la Gaddafi limeomba kuachiliwa kwa wanachama wake, wanaovumilia madhila mengi tu wanayoyapa, kama bara hilo linavyobainisha. Kwa mujibu wa habari zetu, wagombea wa uchaguzi waliokuwa karibu na Saif al-Islam Gaddafi walikamatwa kwa muda nchini Misri (mshirika wa Haftar) kabla ya kuachiliwa.

Kadiri uchaguzi wa Libya unavyokaribia, ndivyo aina ya vita vya kimya kimya kati ya Marshal Haftar na Gaddafi inavyozidi kuongezeka. Iwapo maadhimisho ya tarehe 1 Septemba yalikandamizwa huko Sirte, yalifanyika katika miji mingine kadhaa kama vile Sebha, Bani Walid, au Tarhouna. Hata hivyo maandamano yalifanyika Tunisia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.