Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

Libya: Ujumbe wa jeshi la Urusi wazuru jeshi la ANL la Marshal Haftar

Iousous-bek Bamatguireïevich Evkurov, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi, anaongoza ujumbe wa kijeshi huko Benghazi, kwa mwaliko wa Jeshi la Kitaifa la Libya (ANL) la Marshal Khalifa Haftar, mbbe wa kivita mashariki mwa Libya. Fursa kwa Urusi kuthibitisha uhusiano wake na ANL.

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi Yunus-bek Bamatgirevich Yevkurov wakati wa Kongamano la l Kimataifa la Kiufundi la Kijeshi mwaka 2022' mnamo Agosti 15, 2022, huko Kubinka, nje ya Moscow, Urusi.
Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi Yunus-bek Bamatgirevich Yevkurov wakati wa Kongamano la l Kimataifa la Kiufundi la Kijeshi mwaka 2022' mnamo Agosti 15, 2022, huko Kubinka, nje ya Moscow, Urusi. Getty Images - Contributor
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa maafisa wa kijeshi wa Urusi, ukiongozwa na Naibu Waziri wa Ulinzi, umewasili Benghazi mnamo Agosti 22, 2023 kwa mwaliko wa Marshal Khalifa Haftar, kiongozi wa kivita mashariki mwa Libya.

Ziara hii ya siku mbili itajadili, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi, matarajio ya ushirikiano wa kijeshi katika mapambano dhidi ya ugaidi na "maswala mengine ya hatua za pamoja", taarifa imesema.

Ziara hii ya "kushtukiza" kwa baadhi, "rasmi" kwa wengine, kwa jeshi la kitaifa la Libya (ANL), inakuja saa chache baada ya tangazo lililotolewa na Yevgeny Prigozhin, mkuu wa kikundi cha wanamgambo wa Urusi Wagner, akidai kuwa tena Afrika. "Kutimiza majukumu" na kuifanya "Urusi kuwa kubwa zaidi".

Ikitengwa katika eneo la kimataifa tangu vita vya Ukraine, Moscow inatafuta washirika na kuongeza juhudi na ishara kuelekea nchi za Kiafrika.

Kwa Urusi, Libya ni daraja la mbele kwa uwepo wake barani Afrika na imekuwa ikiongoza mashambulizi ya kidiplomasia katika bara hilo kwa miaka kadhaa. Urusi inafanya ushindaniwa nguvu na nchi Magharibi zenye ushawishi katika Afrika.

Nchini Libya, Urusi inamuunga mkono Marshal Haftar kwa miaka kadhaa na inadumisha uhusiano endelevu naye dhidi ya serikali ya Tripoli, ambayo inaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Ujumbe huu mpya wa ngazi ya juu, ambao uko Benghazi, kwa hiyo unaongozwa na Iousous-bek Bamatguireïevich Evkurov, kiongozi wa zamani wa jamhuri ya Urusi yenye Waislamu wengi ya Ingushetia. Inaboresha uhusiano licha ya shinikizo la Marekani kwa Khalifa Haftar kukata uhusiano na wanamgambo wa Wagner nchini Libya.

Ujumbe huo umekutana na wakuu wa majeshi ya ANL ili kujadili ushirikiano na uratibu wao kuhusu mafunzo na matengenezo ya silaha na vifaa vya Urusi, kulingana na taarifa kutoka kwa ANL.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.