Pata taarifa kuu

Gabon: Wakazi wa Libreville wasubiri kuapishwa kwa Jenerali Oligui Nguema

Siku tano baada ya kumpindua Rais Ali Bongo, Jenerali Brice Clotaire Oligui Nguema anaapishwa kama rais leo asubuhi mjini Libreville. Anaonekana kuanza majukmu yake rasmi kama rais wa nchi huku akiungwa mkono na watu wengi.

Jenerali Brice Oligui Nguema, mjini Libreville mnamo Agosti 16, 2023, wakati wa sherehe zilizotangulia siku ya uhuru wa Gabon iliyoadhimishwa tarehe 17 Agosti 2023.
Jenerali Brice Oligui Nguema, mjini Libreville mnamo Agosti 16, 2023, wakati wa sherehe zilizotangulia siku ya uhuru wa Gabon iliyoadhimishwa tarehe 17 Agosti 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi walipotwaa mamlaka waliapa kukomesha utawala wa Bongo pindi watakaponyakua madaraka.

Walitangaza kutwaa mamlaka ya kijeshi muda mfupi baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliokuwa na utata. Kwa sasa rais huyo amewekwa kizuizini nyumbani kwakwe.

Kiongozi wa upinzani Albert Ondo Ossa, ambaye hivi karibuni aliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba mapinduzi hayo yalikuwa "mapinduzi ya Ikulu", yaliyobuniwa na familia ya Bongo ili kuendelea kuhodhi madaraka yao.

Muungano unaomuunga mkono Bw Ossa, Alternance 2023, ambao unasema ndiye mshindi halali wa uchaguzi wa Jumamosi iliyopita, umehimiza jumuiya ya kimataifa kushinikiza kurejeshwa kwa utawala wa kiraia.

Aliongeza kuwa mpango wa Jenerali Nguema kuapishwa kama rais wa mpito siku ya Jumatatu ni "upuuzi", msemaji wa Bw Ossa, Alexandra Pangha, aliambia BBC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.