Pata taarifa kuu

Niger: Ujumbe wa ECOWAS wakutana na rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum

Siku moja baada ya mkutano huko Accra wa wakuu wa majeshi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), ujumbe kutoka taasisi hii ndogo ya kikanda uliwasili Jumamosi 19 Agosti, huko Niamey.

Ujumbe wa ECOWAS ukikutana na rais wa Niger aliyetimuliwa mamlakani Mohamed Bazoum Jumamosi Agosti 19, 2023.
Ujumbe wa ECOWAS ukikutana na rais wa Niger aliyetimuliwa mamlakani Mohamed Bazoum Jumamosi Agosti 19, 2023. © Nigeria Presidency
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel

Ujumbe kutoka ECOWAS, uliowasili Niamey siku ya Jumamosi saa sita mchana, ulipokelewa kwenye uwanja wa ndege na Waziri Mkuu aliyeteuliwa na viongozi wa mapinduzi, Mahamane Lamine Zeine. Wakiongozwa na rais wa zamani wa Nigeria, Abdulsalami Abubakar, wawakilishi wa jumuiya hiyo ya Afrika Magharibi waliweza kukutana na Rais Mohamed Bazoum, aliyepinduliwa Julai 26.

Mkutano huu ulifanyika mbele ya Waziri Mkuu aliyeteuliwa na viongozi wa mapinduzi na mjumbe mwingine wa utawala huo wa kijeshi, kwa mujibu wa taarifa zetu. Hakuna habari iliyofichuliwa kuhusu mazungumzo yao, wajumbe wa ECOWAS walikuwa wamekuja kuona mazingira ambamo rais aliyepinduliwa anazuiliwa. Ujumbe huu hapo awali ulikutana na wajumbe wa serikali ya kijeshi, akiwemo Jenerali Tiani. walikuwa na ujumbe: kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba nchini Niger. Hatujui kwa sasa majibu ya kiongozi wa mapinduzi.

Kulingana na mmoja wa wajumbe wa ECOWAS, kwa ombi la utawala wa kijeshi, mkutano mwingine na rais wa zamani wa Niger, Mahamat Issoufou, ulijumuishwa katika mpango huo.

Ujumbe huo ulijumuisha tmwenyekitiwa Tume ya ECOWAS. Ni ujumbe huu ambao ulifanya ziara yake ya kwanza kwenda Niamey baada ya mapinduzi. Ulipokelewa vibaya na haukuweza kuondoka kwenye uwanja wa ndege. Kulingana na habari zetu, Rais wa Togo, Faure Gnassingbé, alitekeleza jukumu la busara ili Niamey, wakati huu, ifungue milango yake kwa upana kwa wajumbe kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.