Pata taarifa kuu

Cape Verde: Zaidi ya wahamiaji 60 wafariki baada ya boti yao kuzama

Zaidi ya wahamiaji 60 wanakisiwa kupoteza maisha baada ya boti yao kuzama, ambao uliondoka pwani ya Senegal mapema mwezi Julai na kupatikana kwenye pwani ya Cape Verde siku ya Jumatatu, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema siku ya Jumatano.

Idadi ya waliofariki inakadiriwa kufikia 63, na walionusurika ni 38.
Idadi ya waliofariki inakadiriwa kufikia 63, na walionusurika ni 38. © JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya waliofariki inakadiriwa kufikia 63, na walionusurika ni 38, wakiwemo watoto wanne wenye umri wa kati ya miaka 12 na 16, msemaji wa IOM, Safa Msehli amesema.

Boti hiyo ilionekana Jumatatu katika Bahari ya Atlantiki takriban maili 150 (kilomita 277) kutoka kisiwa cha Cape Verde cha Sal na iligunduliwa na meli ya uvuvi ya Uhispania ambayo ilitahadharisha mamlaka, imesema polisi ya Cape Verde, iliyo kwenye umbali wa kama kilomita mia sita kutoka pwani ya Senegal. .

Watu 56 hawajulikani walipo

Mbali na manusura 38, waokoaji walipata miili ya watu saba waliofariki, amebainisha msemaji huyo.

Kwa mujibu wa shuhuda za manusura walionukuliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Senegal na vyanzo vingine, boti hiyo ilikuwa imeondoka eneo la Fass Boye (magharibi), kwenye pwani ya Senegal, Julai 10 ikiwa na abiria 101.

Hivyo watu 56 hawajulikani walipo. "Kwa kawaida, watu wanaporipotiwa kutoweka kufuatia ajali yaboti, hudhaniwa kuwa wamefariki," amesema msemaji wa IOM, Safa Msehli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.