Pata taarifa kuu

Cape Verde: Wahamiaji 38 waokolewa kwenye mtumbwi, wengi hawajulikani walipo

Kulingana na mamlaka ya Cape Verde na Senegal, watu zaidi ya mia moja walisafiri kwa boti ambayo iliondoka Senegal kwa wiki chache zilizopita.

Waokoaji wa Senegal wanaiopoa miili ya wahanga kufuatia kuzama kwa mtumbwi uliokuwa umebeba wahamiaji wengi, ajali iliyotokea Jumatatu Julai 24, 2023 kwenye pwani ya Dakar.
Waokoaji wa Senegal wanaiopoa miili ya wahanga kufuatia kuzama kwa mtumbwi uliokuwa umebeba wahamiaji wengi, ajali iliyotokea Jumatatu Julai 24, 2023 kwenye pwani ya Dakar. REUTERS - NGOUDA DIONE
Matangazo ya kibiashara

Wahamiaji 37 wa Senegal, pamoja na Bissau-Guinean, waliokolewa Jumatatu Agosti 14 wakiwa kwenye mtumbwi katika pwani ya Cape Verde, mamlaka ya Senegal na Cape Verde wamesema hivi punde Jumanne usiku. Wengine wengi wameangamia, huku hatima ya makumi ya wengine bado haijulikani. Kulingana na shuhuda za walionusurika, boti hiyo iliondoka eneo la Fass Boye (magharibi), kwenye pwani ya Senegal, mnamo Julai 10 "ikiwa na abiria 101", imesema wizara, bila habari zaidi juu ya tukio hilo.

Hapo awali, maafisa mbalimbali wa Cape Verde waliripoti kuhusu manusura arobaini na maiti kadhaa waliopatikana kwenye boti hiyo. Polisi ya Cape Verde, katika taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Facebook, imeripoti habari zilizokusanywa wakati wa uokoaji siku ya Jumatatu kwamba karibu abiria 100 walikuwa wameondoka kutoka pwani ya Afrika Magharibi.

'Muwapokee walio hai na muwazike kwa heshima waliofariki'

Boti hiyo ilionekana kama maili 150 (kilomita 277) kutoka kisiwa cha Cape Verde cha Sal siku ya Jumatatu na meli ya uvuvi ya Uhispania ambayo ilitoa taarifa kwa mamlaka ya Cape Verde, polisi imesema. Afisa wa huduma za afya huko Sal, Jose Rui Moreira, aliripoti manusura 38, saba kati yao walihitaji kulazwa hospitalini. Taasisi hiyo ya uchunguzi imesema ilipokea miili ya watu saba. Huduma zote zenye uwezo zinafanya kazi ili kuwasaidia walionusurika, polisi inasema.

"Lazima tufungue mikono yetu na kuwakaribisha walio hai na kuzika kwa heshimawaliofariki," amesema Waziri wa Afya Filomena Goncalves, aliyenukuliwa na shirika la habari la Inforpress. Wizara ya mambo ya nje ya Senegal, "kwa kushirikiana na mamlaka husika ya Cape Verde, imefanya mipango muhimu ya kuwarejesha makwao (raia wa Senegal) haraka iwezekanavyo", Waziri wa Afya Filomena Goncalves amesema.

Takriban wahamiaji 90 kutoka Senegal, Gambia, Guinea-Bissau na Sierra Leone waliokolewa katika maji ya Cape Verde katikati mwa mwezi Januari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.