Pata taarifa kuu

Mapinduzi nchini Niger: Operesheni za kibinadamu za Umoja wa Mataifa 'zimesitishwa'

Kufuatia mapinduzi hayo, operesheni za kibinadamu za Umoja wa Mataifa nchini Niger "zimesitishwa", msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric ametangaza siku ya Alhamisi.

Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Niger, Niamey.
Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Niger, Niamey. AP - Sam Mednick
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kibinadamu (OCHA), idadi ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu nchini humo imeongezeka kutoka milioni 1.9 mwaka 2017 hadi milioni 4.3 mwaka 2023, na idadi ya watu wenye uhaba mkubwa wa chakula inatarajiwa kufikia milioni 3 kati ya mwezi Juni na Agosti, kabla ya mavuno yajayo.

Wakati huo huo rais wa Niger Mohamed Bazoum ametoa ujumbe wa kuonesha ukaidi kwenye Twitter baada ya wanajeshi kutangaza mapinduzi usiku kucha katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 64, ambaye alichaguliwa kuwa rais wa Niger miaka miwili iliyopita, aliandika kwenye mtandao wa Twitter siku ya Alhamisi asubuhi na kusema: "Mafanikio yaliyopatikana kwa bidii yatalindwa. Wananchi wote wa Niger wanaopenda demokrasia na uhuru watashuhudia hilo."

Waziri wake wa mambo ya nje amesema mapinduzi hayo hayaungwi mkono na jeshi zima, lakini mkuu wa jeshi sasa amesema anaunga mkono utawala wa kijeshi.

Hayo yanajiri wakati Mwenyekiti wa ECOWAS, rais wa Nigeria Bola Tinubu amesema Jumuiya hiyo inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa demokrasia inadumishwa nchini Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.