Pata taarifa kuu

Jumuiya ya ECOWAS yalaani mapinduzi ya kijeshi nchini Niger

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS na Umoja wa Afrika, zimelaani kuzuiwa kwa rais Bazoum na baadaye jeshi kutangaza kuchukua madaraka.

Mwenyekiti wa ECOWAS, rais wa Nigeria Bola Tinubu amesema Jumuiya hiyo inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa demokrasia inadumishwa nchini Niger
Mwenyekiti wa ECOWAS, rais wa Nigeria Bola Tinubu amesema Jumuiya hiyo inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa demokrasia inadumishwa nchini Niger © Wikicommons
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa ECOWAS, rais wa Nigeria Bola Tinubu amesema Jumuiya hiyo inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa demokrasia inadumishwa nchini Niger.

Ufaransa nayo kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya nje Catherine Colonna imelaani kwa nguvu zote hatua hiyo ya Jeshi na kutoa wito kwa ECOWAS na AU kurejesha demokrasia nchini Niger.

Marekani ambayo ni Mshirika wa karibu wa Niger, nayo imelaani hatua hiyo na Waziri wake wa Mambo ya nje Anthony Blinken, amekuwa na kauli hii.

‘‘Tunafuatilia kwa karibu matukio nchini Niger, nilizungumza na rais Bazuom na kumhakikishia kwamba Marekani inamuunga mkono kama rais aliyechaguliwa kihalali kule Niger.’’ amesema Anthony Blinken.

00:30

Waziri wake wa Mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken

Aidha Marekani inataka kiongozi huyo aachilwe huru mara moja na kulaani juhudi zozote za kuchukuliwa madaraka kwa kutumia mabavu.

Washington imeeleza kuendelea kushirikiana na serikali yake pamoja na wadau wengine katika kanda hiyo na kote duniani hadi pale hali itakapotatuliwa kwa njia inayofaa na ya amani.

Msemaji wa Jeshi Kanali Meja Amadou Abdramane Sandjodi, akizungumza usiku wa leo kupitia Televisheni ya taifa, ameeleze sababu za kumpindua rais Bazoum.

‘‘Leo Julai 26,2023, sisi vikosi vya ulinzi na usalama, tumekusanyika ndani ya baraza la kitaifa la kulinda nchi(CNSP) tumeamua kukomesha utawala mnaoufahamau, hii inatokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama, utawala mbovu wa kiuchumi na kijamii.’’ amesema Kanali Meja Amadou Abdramane Sandjodi.

00:43

Msemaji wa Jeshi Kanali Meja Amadou Abdramane Sandjodi

 Jeshi tayari limetangaza kufunga mipaka yote ya nchi na kuwataka wananchi kutotembea nje.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.