Pata taarifa kuu

DRC yasaini Itifaki ya mkataba na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu

DRC na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) zimetia saini Itifaki ya mkataba kuhusu kuimarisha ushirikiano wao ili kupambana dhidi ya kutoadhibiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu huko Kinshasa. Hata hivyo, hakuna tangazo lililotolewa wakati wa kuhitimisha ziara ya mwendesha mashtaka wa ICC nchini DRC.

Karim Khan, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC huko Hague, Septemba 2022.
Karim Khan, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC huko Hague, Septemba 2022. © AP/Peter Dejong
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) wametia saini hati ya makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wao katika mapambano dhidi ya kutoadhibiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, Alhamisi hii, Juni 1. 2023, wakati wa sherehe huko Kinshasa. Kilele cha ziara ya siku nne nchini humo kwa Karim Khan, ambaye alizuru mashariki mwa DRC.

Mnamo tarehe 2 Juni 2023, hakuna taarifa iliyovuja kuhusu maudhui ya mkataba huu. Hakuna tangazo kali kufuatia ziara hii, hakuna safu mpya ya uchunguzi iliyofunguliwa rasmi. Hali ambayo haimaanishi kuwa uchunguzi ho haufanyiki. ICC inaweza kuzuia kupata taarifa kwa madhumuni ya uchunguzi.

Mahakama iliomwa na mamlaka ya Kinshasa kushughulikia kesi kuhusu uhalifu wa vuguvugu la M23. Katika hatua hii, mwendesha mashitaka hakuzungumza lolote.

Karim Khan, kwa upande mwingine, alikumbusha kwamba DRC ilikuwa mojawapo ya faili kongwe zaidi za ICC - iliyofunguliwa mwaka 2004 - kwamba tayari kumekuwa na hatia, katika faili ndogo ya Ituri pekee.

Lakini hakutaja uhalifu wa hivi karibuni na hasa matukio ya Kishishe Novemba 2022, ambayo ripoti hiyo inajadiliwa, lakini ambayo yalisababisha mashirika ya haki za binadamu kuomba uchunguzi wa kimataifa.

Karim Khan alisisitiza kuwa mambo yamefanywa "katika ngazi ya kitaifa" na kuongeza kuwa "suluhisho zaidi lazima zipatikane".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.