Pata taarifa kuu

Bei za vyakyala zang'ata tena Morocco

Nchini Morocco, huku maandamano yakipangwa kufanyika Jumamosi hii, Aprili 8, dhidi ya gharama ya juu ya maisha, raia wanabani kwamba bei ya bidhaa muhimu vya msingi, hasa chakula imepanda maradufu. Katikamji mkuu wa nchi hiyo, Rabat, bei za vyakula vyote zimeongezeka katika miezi ya hivi karibuni, hasa katikati ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Wateja na wafanyabiashara wanatupiana lawama.

Kupanda kwa bei kunawaathiri sana Wamorocco. Hapa, mfanyabiashara anasubiri wateja kwenye kibanda chake huko Rabat, wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kupanda kwa bei kunawaathiri sana Wamorocco. Hapa, mfanyabiashara anasubiri wateja kwenye kibanda chake huko Rabat, wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. © Fadel Senna / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Rabat, Victor Mauriat

Covid-19, vita nchini Ukraine, ukame… Morocco imeathiriwa sana na mzozo wa kiuchumi katika miezi ya hivi karibuni, hasa katika bidhaa za chakula.

Huko Rabat, katika soko kuu la Madina, meneja wa bucha ya Belhaj atapunguza oda zake kwa sababu wateja hununua bidha hiyo kwa kiwango kidogo kuliko kawaida: "Kuna watu walikuwa wananunua kwa mfano kilo 2, sasa wananunua kilo 1. Hawawezi tena kununua kilo hizo 2 kwa sababu bei zimepanda. Bajeti yao ya nyama bado ni ile ile na ndiyo maana kiwango kimepungua”.

Katikati ya mfungo wa Ramadhani, kila jioni ni sherehe

Kwa wastani, bei za vyakula zimepanda kwa asilimia 20 tangu mwaka jana, lakini mboga ndio zimeathirika zaidi. Katika mwezi wa Machi pekee, wafanyabiashara walilazimika kuongeza bei zao kwa zaidi ya 17%, mmoja wa wafanyabiashara anasema: "Mimi, pia, ninapata shida na wateja na hata kwa wauzaji wa jumla. Kununua mboga ni ghali sana. Hata kwa muuzaji wa jumla.

Katikati ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo kila jioni ni sherehe, lakini maka huu hali ni ngumu: "Kila kitu tunachonunua kila siku ni ghali sana. Bei inaongezeka maradufu. Wakati mwingine unapata vitu ambavyo unatakiwa kutumia lakini huwezi kununua. Vitunguu sasa vinauzwa dirham 25 [euro 2.23], viazi vinauzwa dirham 15 [euro 1.34]. Ni ghali kidogo kwa kila mtu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.