Pata taarifa kuu

Waandishi wawili wa habari wa Ufaransa wahukumiwa kwa kujaribu kumtusi Mfalme wa Morocco

Uamuzi huo umetolewa Machi 14, 2023 katika Mahakama ya Jinai ya Paris: wanahabari hao wawili Catherine Graciet na Eric Laurent wamepatikana na hatia ya kujaribu kumtusi Mfalme wa Morocco na wamehukumiwa kifungo cha mwaka 1 jela na faini ya euro 10,000. Mawakili wao wameamua kukata rufaa.

Mfalme wa Morocco Mohammed VI mnamo Novemba 2021.
Mfalme wa Morocco Mohammed VI mnamo Novemba 2021. © Moroccan Royal Palace / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kifungo cha mwaka mmoja na faini ya euro 10,000 kwa kila mmoja wa waandishi wawili wa habari wa Ufaransa, ni hukumu amayo imetolewa na Mahakama ya Jinai ya Paris. Uamuzi huo unaendana na ule uliombwa na ofisi y mashitaka miezi miwili iliyopita. Hatua ya kiraia ya Ufalme wa Morocco pia ilionekana kuwa inakubalika na washtakiwa wawili watalazimika kulipa euro 5,000 kila mmoja kwa Makhzen.

Kwa hivyo hakimu alizingatia kwamba Catherine Graciet na Eric Laurent walitaka kumsaliti Mfalme wa Morocco mnamo 2015 ili kubadilishana na kutochapishwa kwa kitabu cha aibu kwa familia ya kifalme ya Morocco. Kile ambacho wanahabari hao wawili wamekuwa wakikanusha kila mara.

Mawakili wa wanahabari wawili watakata rufaa

Kwa kuamini badala yake kwamba wameangukia katika mtego na usaliti kwa upande wa mamlaka ya kifalme ya Morocco, walimetambua tu kosa la kimaadili: lile la kukubali kupewa euro milioni 2 kutoka Ikulu ya Morocco. ikiwa wtasitisha kuchapisha kitabu chao.

Mawakili wa mfalme wa Morocco wameridhika na uamuzi huo. Kwa upande mwingine, mawakili wa upande wa utetezi mara moja walitangaza kuwa watakata rufaa ili mahakama iangalie tena rekodi ambazo zililetwa dhidi ya wateja wao na ambazo wanaamini kuwa zilighushiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.