Pata taarifa kuu

Nigeria: Kumi na mbili wafariki katika mlipuko karibu na bomba la mafuta

Mlipuko kando na bomba la mafuta lililoharibiwa na wezi wa mafuta umeua watu wasiopungua kumi na mbili Kusini Mashariki mwa Nigeria, polisi wa eneo hilo na shirika moja lisilo la kiserikali wamesema siku ya Ijumaa.

Baada ya mlipuko wa bomba la mafuta, watu wengi wanatafuta ndugu zao.
Baada ya mlipuko wa bomba la mafuta, watu wengi wanatafuta ndugu zao. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Uharibifu wa bomba, kisha vitendo haramu vya usafishaji wa mafuta kuyauza kkinyume cha sheria, sababu za majanga ya ikolojia na ajali mbaya, zimeenea skatik eneo la kusini la Mafuta nchini Nigeria, mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika.

Mlipuko huo ulitokea usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa katika jamii ya Rumuekpe, katika Jimbo la Rivers, ambapo kunapita bomba la mafuta la Trans-Niger Delta (TNP), kulingana na taarifa ya shirika lisilo la kiserikali la Youths and Environmental Advocacy Centre (YEAC). Habari hii imethibitishwa na polisi wa eneo hilo katika taarifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.