Pata taarifa kuu

Nigeria: Atiku Abubakar na Peter Obi kupinga ushindi wa Bola Tinubu

NAIROBI – Nchini Nigeria, waliokuwa wagombea wa urais Atiku Abubakar na Peter Obi, wamejitokeza na kutangaza kuwa watakwenda Mahakamani kupinga ushindi wa Bola Tinubu wa chama tawala cha APC.

Bola Ahmed Tinubu, Rais Mteule wa Nigeria
Bola Ahmed Tinubu, Rais Mteule wa Nigeria © Bayo Onanuga
Matangazo ya kibiashara

Atiku aliyemaliza wa pili katika uchaguzi wa Jumamosi iliyopita, ameelezea uchaguzi huo kama ubakaji wa demokrasia.

“Uchaguzi wa urais wa mwishoni mwa juma lililopita haukuwa wa huru na haki, uchunguzi wetu wa awali umeonyesha kuwa ulikuwa ni uchaguzi ambao haukuendeshwa vizuri.”ameeleza Atiku Abubakar.

Naye Peter Obi, kutoka chama cha Leba, ameapa kuonesha namna alivyoshinda uchaguzi huo, kwa kuonesha udanganyifu ulivyofanyika mbele ya Mahakama.

Rais mteule wa Nigeria Bola Tinubu ametoa wito kwa wapinzani wake kuungana naye kwa ajili ya ujenzi wa taifa, baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa urais uliompa ushindi.

Muhammadu Buhari rais anayemaliza muda wake, amemtaja mrithi wake Bola Tinubu kama mtu anayestahili kuliongoza taifa hilo baada yake kuondoka, Buhari akieleza kuwa ana imani na Tinubu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.