Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Chad: Mapigano kati ya wafugaji na wakulima yasababisha vifo vya watu 11

Takriban watu kumi na mmoja wameuawa siku ya Jumanne nchini Chad, kilomita 600 mashariki mwa mji mkuu N'Djamena, baada ya mzozo kati ya wafugaji na wakulima, afisa mkuu wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP, siku ya Jumanne, kwa sharti la kutotajwa jina.

Mifugo nchini Chad ambako migogoro kati ya wafugaji na wakulima hutokea mara kwa mara.
Mifugo nchini Chad ambako migogoro kati ya wafugaji na wakulima hutokea mara kwa mara. Getty Images/Michael Fay
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano kati ya jamii hizo mbili yalianza siku ya Jumatatu katika kitongoji kidogo cha Mangalmé kufuatia wizi wa ng'ombe, chanzo hicho kimesema.

Mwezi Agosti, watu 22 waliuawa katika makabiliano kama hayo kati ya wakulima na wafugaji kilomita 500 kusini mwa mji wa N'Djamena. makabiliano haya ya mara kwa mara kwa ujumla unahusisha wafugaji wa kuhamahama wa Kiarabu dhidi ya wakulima wa kiasili wasiofanya kazi ambao wanashutumu wafugaji kwa kupora mashamba yao kwa minajili ya kulisha mifugo yao huko.

Vurugu kati ya jamii hizi hutokea mara kwa mara katikati na kusini mwa nchi, lakini pia mashariki, ambako wakazi wengi wana silaha. Mabedui hao kwa ujumla hutoka katika maeneo kame ya Sahel kaskazini mwa Chad na wanataka kuendelea kukaa kwenye ardhi yenye rutuba inayofaa kufuga ngamia na kondoo wao hasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.