Pata taarifa kuu
AMANI-SIASA

Waasi wa zamani wa Kongo wadai hadhi rasmi ya kiongozi wao

Wafuasi wa kiongozi wa zamani wa waasi Frédéric Bintsamou, almaarufu Mchungaji Ntumi, wanaomba mamlaka ya Kongo kutoa nafasi rasmi kwa kiongozi wao, kwa mujibu wa makubaliano ambayo yalimaliza mzozo wa kivita ambao ulitikisa eneo la Pool, kusini mwa nchi kati ya mwaka 2016 na 2017.

Mchungaji Frédéric Bintsamou almaarufu "Ntumi" Juni 20, 2007 katika mji wa Kinkala kusini mwa Congo.
Mchungaji Frédéric Bintsamou almaarufu "Ntumi" Juni 20, 2007 katika mji wa Kinkala kusini mwa Congo. AFP
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya miaka mitano baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, "hakuna ishara kubwa kutoka kwa upande wa serikali kuamua hadhi (yake)", Ané Philippe Bibi, anayesimamia chama cha upinzani cha CNR, chama kinachoongozwa na Mchungaji Ntumi ameliambia shirika la habari la AFP. "Kiongozi wetu lazima awe wa kwanza kupewa nafasi muhimu au kupewa hadhi kubwa (...) hadhi yake lazima ibainishwe, sanjari na kuwarejesha wapiganaji wa zamani katika maisha ya kiraia au kuingizwa katika vikosi vya usalama na ulinzi", amesisitiza.

Mchungaji Ntumi na wapiganaji wake wa zamani wa 'ninja' ambao walishiriki katika mzozo wa awali wa Pool kati ya 1998 na 2003 waliopinga kuchaguliwa tena kwa Rais Denis Sassou Nguesso 2016, walichukua silaha dhidi ya utawala wa Brazzaville.

Makubaliano ambayo yalimaliza mgogoro huo mwishoni mwa mwaka 2017 yalitoa, pamoja na mambo mengine, kwa ufafanuzi wa hadhi maalum ya Bw. Ntumi, kupokonywa silaha na kuingizwa katika vijkosi vya usalama na ulinzi kwa wapiganaji wa zamani ili 'kuimarisha amani'.

Tangu wakati huo, Bw. Ntumi anaishi katika ngome yake ya Pool, eneo lenye rutuba kwa muda mrefu ambalo lilizingatiwa kuwa kikapu cha mkate cha Brazzaville, wakati serikali inadai kukusanya na kuharibu angalau silaha 8,000.

Baada ya mzozo wa kwanza wa Pool, Bwana Ntumi alishika wadhifa wa "mjumbe mkuu anayesimamia kukuza maadili ya amani na ukarabati wa matokeo ya vita" katika ofisi ya Mkuu wa Nchi, aina ya wadhifa ambao wafuasi wake wanadai apewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.