Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Sudan: Nchi za Magharibi na Urusi zazidisha ushawishi wao

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov yuko Sudan leo Alhamisi Februari 9, siku moja baada ya ziara ya wawakilishi wa Marekani, Ufaransa, Norway, Uingereza na Ujerumani, pamoja na wale wa Umoja wa Ulaya. Khartoum ni uwanja wa ziara ya kweli ya kidiplomasia kati ya nchi za Magharibi na Urusi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, anayeongoza Sudan, Februari 9, 2023 mjini Khartoum.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, anayeongoza Sudan, Februari 9, 2023 mjini Khartoum. via REUTERS - RUSSIAN FOREIGN MINISTRY
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Mauritania na Mali, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi yuko Sudan. Sergueï Lavrov anatarajia kukutana na mamlaka za kijeshi nchini humo,  mkuu wa utawala wa kijeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake, Jenerali Hemidti.

Ziara hii inakuja wakati, saa 24 mapema, wajumbe kutoka nchi tano za Magharibi - Marekani, Ufaransa, Norway, Uingereza na Ujerumani - pamoja na wale kutoka Umoja wa Ulaya (EU) pia walikuwa walizuru Khartoum.

Hii sio bahati mbaya, anasisitiza mtafiti: Urusi na nchi za Magharibi wanapigania ushawishi katika eneo hilo.

Shinikizo la Magharibi kwa ajili ya mpito kuelekea demokrasia

Wakati wa ziara yao ya siku mbili, wawakilishi wa nchi za Magharibi walitaka kuhakikisha kuwa serikali ya Sudan bado inaunga mkono mabadiliko ya demokrasia.

Kama ukumbusho, mwanzoni mwa mwezi Desemba, wanajeshi waliokuwa madarakani mjini Khartoum na vyama vikuu vya kisiasa na makundi yanayounga mkono demokrasia walitia saini makubaliano ya awali ambayo yatapelekea kuanzishwa kwa serikali ya kiraia katika miezi ijayo.

Lakini katika siku za hivi karibuni, wanajeshi wamezidisha taarifa zenye utata, wakipendekeza kwamba hawatakubali makubaliano ya kuidhinisha kurejea kwa raia mamlakani.

Mbele ya ujumbe wa Umoja wa Ulaya na Marekani, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan jana hatimaye alisisitiza dhamira yake ya mpito kuelekea demokrasia.

Watu wa Magharibi wana wasiwasi juu ya ushawishi unaokua wa Urusi

Kwa ziara hii, anaamini mtafiti huyo, nchi za Magharibi pia zinatafuta kumuunga mkono al-Burhan dhidi ya mpinzani wake, kiongoz nambari mbili wa utawala wa kijeshi, Jenerali Hemidti, aliye na ukaribu na Urusi.

Nchi za Magharibi zina wasiwasi juu ya ushawishi unaokua wa Moscow katika eneo hilo. Na hasa uwepo wa kundi la wanamgambo wa Kirusi la Wagner huko Darfur na katika nchi jirani.

Kabla ya kuwasili Khartoum, waziri wa mambo ya nje wa Urusi alikuwa mjini Bamako ambako aliahidi kuwa Urusi itaendelea kuisaidia Mali kuboresha uwezo wake wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.