Pata taarifa kuu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov kuanza ziara yake Afrika Kusini

Afrika Kusini inampokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov leo Jumatatu, Januari 23, ambaye atakutana na mwenzake, Naledi Pandor. 

Muda mfupi kabla ya ziara ya mkuu wa diplomasia ya Urusi huko Pretoria, Urusi na China zilitangaza kuwa zitashiriki maoezi ya pamoja ya kijeshi karibu na pwani ya Afrika Kusini kwenye Bahari ya Hindi. Hapa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov wakati wa mkutano na waandishi wa habari mnamo Januari 18, 2023.
Muda mfupi kabla ya ziara ya mkuu wa diplomasia ya Urusi huko Pretoria, Urusi na China zilitangaza kuwa zitashiriki maoezi ya pamoja ya kijeshi karibu na pwani ya Afrika Kusini kwenye Bahari ya Hindi. Hapa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov wakati wa mkutano na waandishi wa habari mnamo Januari 18, 2023. © Alexander Zemlianichenko / AP
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya waziri wa Urusi inahakikisha kurejea kwa Urusi katika bara la Afrika baada ya ziara yake nchini Misri, Congo-Brazzaville, Uganda na Ethiopia mwezi Julai mwaka uliopita. 

Afrika Kusini ni mshirika mkubwa, kwa sababu Pretoria inasema haiegemei upande wowote katika mzozo wa Ukraine na imekataa katu katu kulaani uvamizi wa Urusi, karibu mwaka mmoja baada ya kuanza kwa vita.

Serguei Lavrov na Naledi Pandor hatimaye wataweza kuzungumza ana kwa ana baada ya mazungumzo ya simu mwezi Agosti mwaka jana. Baada ya mazungumzo yao, Urusi ilisifu "nafasi ya uwajibikaji ya Pretoria" ambayo inakataa kuipa kisogo Moscow licha ya shinikizo kutoka kwa nchi za Magharibi.

Marekani pia ililaani dhidi ya mazoezi ya pamoja kijeshi yatakayojumuisha majeshi ya wanamaji kutoka Afrika Kusini, China na Urusi yatakayo fanyika mwezi Februari mwaka huu nchini Afrika Kusini. Mafunzo haya si mapya, lakini yanaangukia katika ukumbusho kamili wa mwaka mmoja wa vita nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.