Pata taarifa kuu

Utekaji nyara katika kituo cha treni nchini Nigeria: mateka wa mwisho waachiliwa

Mateka wawili wa mwisho katika utekaji nyara katika kituo cha treni nchini Nigeria wameachiliwa na vikosi vya usalama ambavyo vimewakamata watu saba, wakiwemo wakuu wawili wa vijiji, mamlaka imesema.

Abiria wakiingia kwenye treni ndogo ya Shirika la Reli la Nigeria kwenye Kituo cha Oshodi huko Lagos, Septemba 23, 2016.
Abiria wakiingia kwenye treni ndogo ya Shirika la Reli la Nigeria kwenye Kituo cha Oshodi huko Lagos, Septemba 23, 2016. AFP PHOTO / PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Makumi ya watu waliokuwa wakisubiri treni yao katika jimbo la Edo kuelekea Wari, kusini mwa nchi, walitekwa nyara wakati kituo cha treni kilipovamiwa Januari 7 na watu waliokuwa na silaha. Siku ya Jumapili, Afisa Habari wa Jimbo la Edo Chris Osa Nehikhare alitangaza kuachiliwa kwa mateka 12 kati ya 14 waliosalia.

Mateka wawili wa mwisho wameachiliwa na watu saba kukamatwa, amesema katika taarifa yake siku ya Jumatano. Wawili kati yao walikuwa vikongozi wa kimila. Hapo awali, mateka 32 waliripotiwa kutekwa, lakini idadi hii ilirekebishwa hadi 20.

Kesi hii ya hivi punde ya hadhi ya juu imeangazia kuenea kwa ukosefu wa usalama nchini Nigeria, jambo ambalo litakuwa suala muhimu katika uchaguzi wa mwishoni mwa mwezi Februari kuchukua nafasi ya Rais Muhammadu Buhari. Bwana Buhari, kamanda wa zamani wa jeshi na kiongozi wa zamani wa kijeshi ambaye aliahidi kuifanya Nigeria kuwa salama zaidi, hatowania tena, baada ya mihula miwili na rekodi inayoonekana kuwa ya janga, huku nchi ikiwa katika mzozo mkubwa wa kiuchumi na ukosefu wa usalama.

Utekaji nyara ni jambo la kawaida nchini Nigeria, kwa kawaida hufanyika katika majimbo ya kaskazini-magharibi na kati ya nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika. Lakini vurugu zimeenea katika mikoa mingine.

Mnamo mwezi Machi 2022, watu wenye silaha walilipua sehemu ya njia ya reli kati ya mji mkuu, Abuja na Kaduna (kaskazini), na kuua watu wanane na kuwateka nyara makumi ya abiria, walioachiliwa kwa miezi iliyofuata kwa fidia. Huduma ya reli ilianza tena shughuli zake mnamo Desemba baada ya kuachiliwa kwa mateka wa mwisho.

Nigeria, nchi yenye wakazi milioni 215, sawa na Brazili, iko hatarini: makundi yenye silaha yanaharibu kituo hicho na kaskazini-magharibi, makundi ya wanajihadi yanapamba moto kaskazini-mashariki na kusini-mashariki inaathiriwa na ghasia za kujitenga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.