Pata taarifa kuu
NIGERIA - USALAMA

Kasisi wa kanisa katoliki ameuawa Nigeria na watu wenye silaha

Kasisi wa kanisa katoliki ameuawa na watu wenye silaha katika parokia yake kaskazini mwa Nigeria, na kisha baadae watu hao kuteketeza moto kanisa lake katika kijiji cha Kafin Koro nchini humo.

Ramani ya Nigeria
Ramani ya Nigeria AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwili wa Padre Isaac Achi ulipatikana katika magofu yaliyoteketea ya jengo hilo.

Kasisi mwingine, Padre Collins Omeh, alipigwa risasi alipokuwa akijaribu kuuepuka moto huo ambapo kwa sasa anapokea matibabu hospitalini.

Kwa mujibu wa Padre Collins Omeh, Padre mwenzake aliuawa kwa kupigwa risasi na magaidi hao,waliosikika  wakipiga kelele za kijihadi.

Watu wenye silaha wamekuwa wakiwashambulia raia nchini Nigeria karibu na mpaka wa Niger huku wakiwateka nyara wengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.