Pata taarifa kuu
SIASA-USALAMA

Watatu washtakiwa kwa mapinduzi nchini Gambia

Serikali ya Gambia siku ya Jumanne iliwashtaki raia wawili na afisa wa polisi kuhusiana na jaribio la mapinduzi ya Desemba, msemaji wa serikali amesema katika taarifa.

Wanajeshi wa Senegal kutoka ECOWAS waliotumwa nchini Gambia.
Wanajeshi wa Senegal kutoka ECOWAS waliotumwa nchini Gambia. AFP - CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya nchi hii ndogo ya Afrika Magharibi inayozungumza Kiingereza ilisema tarehe 21 Desemba kwamba ilizima mapinduzi ya kijeshi. Baadaye ilieleza kwamba waliokuwa walianda mapinduzi hayo, walipanga "kuwakamata maafisa wakuu wa serikali na kuwatumia kama mateka ili kuzuia nchi za kigeni kuingilia kati kijeshi".

Raia wawili, Mustapha Jabbi na Saikuba Jabbi, na inspekta wa polisi Fakebba Jawara walikamatwa mnamo Desemba 30 na kushtakiwa kwa kuficha uhaini na kula njama ya kutenda uhalifu, imesema taarifa hiyo. Takriban wanajeshi saba tayari wamekamatwa kuhusiana na kesi hii.

Kwa upande mwingine, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Unified Democratic Party (UDP), waziri chini ya udikteta wa Yahya Jammeh (1994-2017), Momodou Sabally, aliachiliwa huru wiki iliyopita, siku chache baada ya kukamatwa kwake baada ya kuonekana kwenye video inayopendekeza kuwa Rais Adama Barrow, aliyechaguliwa tena mwaka mmoja uliopita, ataondolewa madarakani kabla ya uchaguzi ujao.

Tume ya uchunguzi, inayotarajiwa kuripoti mwishoni mwa mwezi huu, imeundwa ili kutoa mwanga juu ya jaribio hili la kijeshi, ambalo ni la hivi punde zaidi katika Afrika Magharibi tangu 2020, baada ya kufanikiwa mara mbili nchini Mali na Burkina Faso, nyingine nchini Guinea , na jaribio lingine la mapinduzi huko Guinea-Bissau.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.