Pata taarifa kuu

Gambia yazima jaribio la mapinduzi

Serikali ya Gambia imesema Jumatano kwamba jaribio la mapinduzi ya kijeshi lilishindwa siku moja kabla na wanajeshi wanne walikamatwa.

Picha inayoonyesha vikosi vya usalama vya Gambia vilivyotumwa Banjul, Desemba 5, 2016.
Picha inayoonyesha vikosi vya usalama vya Gambia vilivyotumwa Banjul, Desemba 5, 2016. AP - Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya nchi ndogo zaidi katika bara la Afrika imehakikishia katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba hali "imedhibitiwa kabisa". Hakuna uthibitisho uliopatikana kutoka kwa chanzo chochote isipokuwa taarifa ya serikali.

Taarifa nadra za wanajeshi waliokuwa wakizunguka makao makuu ya rais katikati mwa mji mkuu Banjul siku ya Jumanne jioni, na uvumi ulienea usiku kucha kuhusu jaribio la mapinduzi katika nchi hiyo ambayo mwaka 2017 iliingia katika utawala dhaifu wa kidemokrasia baada ya zaidi ya miaka ishirini ya udikteta chini ya utawala wa Yahya Jammeh.

Serikali ya Gambia inatangaza kuwa, kulingana na taarifa za kiintelijensia zinazoonyesha kuwa baadhi ya wanajeshi wa jeshi la Gambia walikuwa wakipanga njama ya kupindua serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya Rais Adama Barrow, amiri jeshi mkuu wa jeshi la Gambia, ilifanya operesheni ya kijeshi haraka jana na kuwakamata wanajeshi wanne wanaohusishwa na jaribio hili la mapinduzi,” Ebrima G. Sankareh, msemaji wa serikali na mshauri wa rais ameandika katika taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Askari hao wanne wanahojiwa na polisi wa kijeshi na washirika watatu wanatafutwa, amesema. "Serikali inawataka wananchi, wakazi na mabalozi kufanya shughuli zao kama kawaida; hali imedhibitiwa kikamilifu na hakuna haja ya kuwa na hofu," amesema.

Hatua ya kushtukiza ya Adama Barrow kushika wadhifa wa urais mnamo Januari 2017 ilimaliza miongo miwili ya utawala wa kiimla katika nchi hii ndogo, maskini yenye watu milioni mbili. Bw. Barrow kwa kiasi kikubwa alishinda muhula wa pili mwezi Desemba 2021 wakati wa uchaguzi wa rais.

Washirika wa kimataifa wa Gambia, hata hivyo, wanashinikiza kuwepo kwa mageuzi makubwa ili kuimarisha demokrasia. Yahya Jammeh, aliye uhamishoni, anaendelea kuwa na ushawishi mkubwa nchini humo. Viongozi wa Afrika Magharibi wana wasiwasi kuhusu athari za mapinduzi ya kijeshi katika eneo hilo.

Wakikutana katika mkutano wa kilele mapema mwezi wa Desemba mjini Abuja, waliamua kuunda kikosi cha kikanda kilichojitolea kuingilia kati sio tu dhidi ya wanajihadi lakini pia katika tukio la mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.