Pata taarifa kuu
HAKI-MAANDAMANO

Maandamano mabaya nchini Chad: Watoto 80 waachiliwa kwa dhamana

Jumla ya watoto 80, waliofunguliwa mashitaka kwa madai ya kuhusika katika maandamano ya umwagaji damu yaliyokandamizwa mwezi Oktoba nchini Chad, wameachiliwa kwa dhamana baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu, mwendesha mashtaka wa jamhuri katika mji wa N' Djamena amesema.

Watoto hao 80 walikamatwa huko N'Djamena wakati na baada ya maandamano dhidi ya serikali mnamo Oktoba 20 ambayo yalisababisha vifo vya takriban watu hamsini, wakati maafisa wa polisi walipofyatua risasi dhidi ya umati wa watu waliokuwa wakijaribu kukusanyika.
Watoto hao 80 walikamatwa huko N'Djamena wakati na baada ya maandamano dhidi ya serikali mnamo Oktoba 20 ambayo yalisababisha vifo vya takriban watu hamsini, wakati maafisa wa polisi walipofyatua risasi dhidi ya umati wa watu waliokuwa wakijaribu kukusanyika. AP
Matangazo ya kibiashara

"Ombi la kuachiliwa kwa dhamana kwa niaba yao limewasilishwa na jaji alikubali ombi hili," mwendesha mashtaka Moussa Wade Djibrine ameliambia shirika la habaria la AFP, na kuongeza kuwa "uchunguzi unaendelea".

Siku ya Jumatatu, Bw. Djibrine alitangaza kuwahukumu watu 262 kifungo baada ya kesi ya watu 401 waliokuwa wakishikiliwa kwa siku nne katika jela ya Koro Toro, kilomita 600 kaskazini mashariki mwa mji mkuu.

Watoto hao 80 walikamatwa huko N'Djamena wakati na baada ya maandamano dhidi ya serikali mnamo Oktoba 20 ambayo yalisababisha vifo vya takriban watu hamsini, wakati maafisa wa polisi walipofyatua risasi dhidi ya umati wa watu waliokuwa wakijaribu kukusanyika.

Mnamo Oktoba 20, waandamanaji waliitikia wito wa upinzani dhidi ya kuongezwa kwa miaka miwili madarakani kwa Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno. Alitangazwa kuwa mkuu wa nchi na jeshi mnamo Aprili 20, 2021 kufuatia tangazo la kifo cha babake, Rais Idriss Déby Itno, aliyeuawa na waasi katika uwanja wa mapigano baada ya kuongoza Chad kwa mkono wa chuma kwa miaka 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.