Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Watu 11 wajeruhiwa katika shambulizi dhidi ya msikiti kusini mwa Nigeria

Watu wenye silaha wameshambulia msikiti mmoja kusini mwa Nigeria siku ya Ijumaa wakijaribu kumteka nyara imamu bila kufanikiwa lakini wakiwapiga risasi waumini kumi na mmoja, polisi wa eneo hilo imeliambia shirika la habari la AFP.

Vyombo vya habari vya eneo hilo, vikimnukuu kiongozi wa jamii na mmoja wa waliojeruhiwa, vinaripoti kwamba mmoja wa maimamu alitekwa nyara na washambuliaji. Lakini polisi walikanusha habari hii, na kuongeza: "Ilikuwa nia yao kumkamata, lakini hawakufanikiwa". Sababu hasa za shambulio hili bado hazijajulikana.
Vyombo vya habari vya eneo hilo, vikimnukuu kiongozi wa jamii na mmoja wa waliojeruhiwa, vinaripoti kwamba mmoja wa maimamu alitekwa nyara na washambuliaji. Lakini polisi walikanusha habari hii, na kuongeza: "Ilikuwa nia yao kumkamata, lakini hawakufanikiwa". Sababu hasa za shambulio hili bado hazijajulikana. REUTERS/Seun Sanni
Matangazo ya kibiashara

Msikiti wa Ughelli, mji unaopatikana katika Jimbo la Delta, umelengwa wakati wa sala ya asubuhi na watu wenye silaha. "Waumini kumi na moja wamejeruhiwa katika shambulio hili," msemaji wa Polisi wa Jimbo la Delta Bright Edafe amesema.

"Hadi sasa, hatujakamata mtu yeyote, lakini niwakuhakikishia kuwa tutawakamata waliohusika na shambulio hili," ameongeza.

Vyombo vya habari vya eneo hilo, vikimnukuu kiongozi wa jamii na mmoja wa waliojeruhiwa, vinaripoti kwamba mmoja wa maimamu alitekwa nyara na washambuliaji. Lakini polisi walikanusha habari hii, na kuongeza: "Ilikuwa nia yao kumkamata, lakini hawakufanikiwa". Sababu hasa za shambulio hili bado hazijajulikana.

Visa vya utekaji nyara hutokea mara kwa mara katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika, iliyokumbwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na kukabiliwa na ukosefu wa usalama wa jumla, kati ya mashambulizi ya wahalifu na makundi ya kijihadi.

Ni katika hali hii ya wasiwasi ambapo wapiga kura wa Nigeria wanaitwa kupiga kura mnamo Februari 25 kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, ambaye anajiuzulu baada ya mihula miwili, kama ilivyoainishwa katika Katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.