Pata taarifa kuu

Mkutano wa 18 wa La Francophonie wakumbwa na mvutano mkali kati ya Rwanda na DRC

Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa, Francophonie (OIF) linakaribia kumalizika mkutano wake wa 18 huko Djerba, Tunisia. Wakuu wa nchi na serikali wamejadili mgogoro wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Azimio linatarajiwa kuchukuliwa juu ya suala hili, lakini ni dhahiri kuwa, jumuiya hiyo inakabiliwa na mvutano mkali.

Rais wa Tunisia Kais Saied akizungumza wakati wa Mkutano wa 18 wa Francophonie mjini Djerba, Tunisia, Novemba 19, 2022.
Rais wa Tunisia Kais Saied akizungumza wakati wa Mkutano wa 18 wa Francophonie mjini Djerba, Tunisia, Novemba 19, 2022. via REUTERS - TUNISIAN PRESIDENCY
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwanzo wa mkutano huu, mvutano ulionekana. Kwa upande wa wajumbe wa Kongo,  wanadai kwamba kuna upendeleo wa katibu mkuu wa OIF, Louise Mushikiwabo, ambaye ni raia wa Rwanda.

"Ametoka kidogo katika msimamo wake wa kutoegemea upande wowote", alituambia, Jumapili asubuhi, mmpoja wa wajumbe wa Kongo ambaye anamtuhumu Louise Mushikiwabo kwa kuficha "ukweli na kuipendelea Rwanda", na hivyo kumshutumu waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje wa Rwanda kwamba jumuiya anayoongoza haiwezi kuwa na jukumu kwa kutatua mgogoro huo”.

Maneno haya yanahusu mahojiano ambayo katibu mkuu aliyatoa kwa wenzetu wa TV5, siku ya kwanza ya mkutano huo. Louise Mushikiwabo alisema katika mahojiano haya kwamba kuna "askari wa DRC, kwenye mpaka na Rwanda, ambao ni tishio kwa usalama wa Rwanda".

Maneno ambayo hayakupokelewa vema kwa upande wa Kongo. "Tulieleza kwa kifupi kwamba kama Katibu Mkuu, Louise Mushikiwabo ana jukumu la kutoegemea upande wowote na kwamba katika masuala yanayoihusu Rwanda, hata kama ni Mnyaradwa, hangepaswa kuegemea upande wowote," Waziri Mkuu wa Kongo Sama Lukonde ameiambia RFI.

Hivyo, akikabiliwa na tuhuma za upendeleo, msemaji wa Katibu Mkuu, Oria Vande weghe, amesema: "Ndiyo, Louise Mushikiwabo alikuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi yake, lakini leo sivyo. Anawakilisha nchi 88 na serikali. Hakika ni ngumu kueleza, lakini ni ukweli anaoongea, " amebaini.

Ikumbukwe kwamba Rais wa DRC, Félix Tshisekedi hakushirikimkutano huo, ingawa DRC ndiyo nchi kubwa zaidi ya La Francophonie. "ni ujumbe ambao tulitaka kutuma na tutaendelea kutuma ujumbe wa aina hii", amesema mmoja wa wajumbe wa DRC katijka mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.