Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron ataka kuungwa mkono katika mkutano wa Francophonie Djerba, Tunisia

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anashiriki, Jumamosi, Novemba 19, katika mkutano wa kilele wa La Francophonie huko Djerba nchini Tunisia, ambapo viongozi wa jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa wanakutana. Anashiriki mkutano huo akirejea kutoka Bangkok, ambako alikuwa ameshiriki katika mkutano wa kilele wa APEC, na baada ya mkutano wa mataifa tajiri duniani (G20) huko Bali. Rais Macron anakamilisha operesheni kubwa ya kidiplomasia katika ngazi ya kimataifa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anashiriki mkutano wa kilele wa La Francophonie baada ya ule wa APEC, huko Bangkok, hapa ilikuwa Novemba 18, 2022.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anashiriki mkutano wa kilele wa La Francophonie baada ya ule wa APEC, huko Bangkok, hapa ilikuwa Novemba 18, 2022. © AP - Rungroj Yongri
Matangazo ya kibiashara

Katika kipindi cha wiki mbili, Emmanuel Macron alishiriki mkutano wa Tabia nchi (COP27) huko Misri, mkutano wa nchi tajiri duniani (G20) nchini Indonesia, kongamano la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia-Pasifiki (Apec) nchini Thailand, na kwa sasa yuko Tunisia kwa mkutano wa Francophonie: hatua ya mwisho ya safari ndefu ya kidiplomasia.

Na huko Djerba pia, rais wa Ufaransa ananuia kuzungumzia suala la vita vya Ukraine, katika kikao cha majadiliano cha mlango wa karibu kinachohusu mustakabali wa La Francophonie. Hii ni kwa lengo la kuhamasisha juu ya maadili yaliyoshirikiwa na wanachama wa jumuiya inayozungumza Kifaransa: jumuiya ya La Francophonie inaweza kuwa na jukumu la ushawishi, wazaidizi wa rais Macron wamebainiha.

Emmanuel Macron hatatoa hotuba na hatakaa hadi mwisho wa mkutano huo, kwani amepanga kurejea Ufaransa jioni. Kwa hivyo Rais wa Jamhuri atachukua fursa ya ziara yake huko Djerba kufanya mazungumzo ya nchi mbili na viongozi wenzake wanaozungumza Kifaransa: Rais wa Tunisia na mwenyeji wa mkutano huo Kaïs Saïed, lakini pia na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinian na bila shaka viongozi wa Afrika.

Katika ikulu ya Élysée, inaelezwa kuwa nafasi imehifadhiwa kuandaa majadiliano haya: kabla ya kurejea Paris, Emmanuel Macron bado anataka kujaribu kupata uungwaji mkono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.