Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Mapigano kati ya wafugaji na wakulima yaua watu 18 nchini Nigeria

Watu 18, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, wameuawa katika ghasia za kikabila kati ya wafugaji na wakulima katika jimbo la Benue, katikati mwa Nigeria, maafisa wamesema.

Nchini Nigeria, wakulima wa Bachama wanadaiwa kushambulia vijiji vya wafugaji wa Fulani.
Nchini Nigeria, wakulima wa Bachama wanadaiwa kushambulia vijiji vya wafugaji wa Fulani. Godong/UIG via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Ghasia hizo zilizuka mapema Jumatano wiki hii. Wafugaji walivamia kijiji cha wakulima cha Gbeji wilayani Ukum, wakifyatua risasi kiholela, amesema Paul Hemba, mshauri wa usalama wa gavana wa jimbo la Benue.

Migogoro kati ya wafugaji na wakulima kuhusu ardhi, malisho na haki ya maji ni hutokea mara nyingi tu katika mikoa ya kati na kaskazini magharibi mwa Nigeria.

"Kulingana na ripoti ya hivi punde niliyopokea, watu 18 waliuawa katika shambulio hilo, polisi wawili na wanakijiji 16," Hemba amesema. Watu wengine kadhaa walijeruhiwa na kulazwa hospitalini.

Kamishna wa Polisi wa Jimbo la Benue Wale Abbas amesema ni tukio hilo ni laulipizaji kisasi kufuatia mauaji ya wafugaji watano kutoka jamii ya Fulani waliouawa na wakazi wa eneo hilo. "Mgogoro huo ulianza Jumanne wakati wafugaji watano kutoka jamii ya Fulani walipovamiwa na kuuawa katika matukio matatu tofauti na ng'ombe wao kuibiwa," afisa huyo amesema.

Bw. Abbas ametoa idadi ya waliouawa ikiwa ni chini ya kumi, ikiwa ni pamoja na afisa wa polisi, wakazi na wafugaji. "Afisa wa polisi aliyekufa aliuawa kwa risasi hewa na kufariki akiwa njiani kupelekwa hospitalini," Abbas amesema.

Mivutano ya kikabila wakati mwingine huchukua mwelekeo wa kikabila na kidini nchini Nigeria, ambayo ina makabila kadhaa na imegawanywa kati ya kusini yenye Wakristo wengi na kaskazini yenye Waislamu wengi.

Kaskazini-magharibi na katikati mwa Nigeria pia wameathiriwa pakubwa na ghasia kutoka kwa magenge ya wahalifu wanaojulikana kama "majambazi", ambao huvamia vijiji, kuua na kuchoma nyumba baada ya kuwapora na kujihusisha na utekaji nyara ili kujipatia fedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.