Pata taarifa kuu

Mafuriko Nigeria: Watu 600 wafariki na milioni 1.3 wayatoroka makazi tangu Juni

Ripoti ya kwanza iliyochapishwa wiki iliyopita ilibaini watu 500 walifariki kutokana na mafuriko yaliyokumba baadhi ya maneo nchini Nigeria. Zaidi ya nyumba 82,000 na hekta 110,000 za mashamba pia zimeharibiwa kabisa.

Mafuriko nchini Nigeria yamevunja barabara, na kuwalazimu wakazi wengi kutumia boti kufika maeneo salama.
Mafuriko nchini Nigeria yamevunja barabara, na kuwalazimu wakazi wengi kutumia boti kufika maeneo salama. AP - Fatai Campbell
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watu 600 wamefariki dunia tangu mwezi Juni kutokaa na mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini Nigeria katika muongo mmoja yaliyosababishwa na mvua za yingi, na kuwalazimu watu milioni 1.3 kukimbia makazi yao, kulingana na ripoti mpya kutoka kwa mamlaka.

Tangu kuanza kwa msimu wa mvua, maeneo mengi ya nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika yamekumbwa na mafuriko na hivyo kuzua hofu ya hali kuzidi kuwa mbaya kwa ukosefu wa chakula na mfumuko wa bei.

"Kwa bahati mbaya, zaidi ya watu 603 wamepoteza maisha" - zaidi ya 100 wamekufa katika kipindi cha wiki moja - na watu wengine 2,400 wamejeruhiwa kutokana na mafuriko, Wizara ya Masuala ya Kibinadamu ya Nigeria ilisema Jumapili kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Idadi ya vifo imeongezeka, huku majimbo mengi nchini Nigeria yakishindwa kujiandaa kwa mvua hiyo kubwa, wizara hiyo imesema.

Idadi ya hapo awali ya mamlaka iliyochapishwa wiki iliyopita iliripoti kuwa watu 500 walifariki.

Zaidi ya nyumba 82,000 na hekta 110,000 za mashamba pia ziliharibiwa kabisa, wizara imeongeza.

Msimu wa mvua kwa kawaida huanza mwezi Juni, lakini mafuriko yamekuwa mabaya sana tangu mwezi Agosti, kulingana na dara ya kushughulikia majanga (Nema).

Wiki iliyopita, watu 76 walikufa katika ajali ya boti katika jimbo la Anambra (kusini-mashariki), wakati mafuriko ya Mto Niger yaliposababisha boti hiyo kuzama.

Mvua kubwa inatarajiwa kunyesha tena nchini Nigeria katika wiki zijazo, na kuongeza hofu ya uharibifu zaidi.

Waziri wa Masuala ya Kibinadamu Sadiya Umar Farouq ametoa wito wa kuondolewa kwa watu wanaoishi kando ya mito, hasa katika majimbo ya Anambra, Bayelsa, Cross River, Delta na Rivers, ambayo yanakabiliwa na hatari kubwa ya mafuriko.

Mnamo 2012, mafuriko makubwa yalisababisha vifo vya watu 363 na milioni 2.1 kuhama makazi yao.

Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa unaathiŕika zaidi na mabadiliko ya Tabia nchi na chumi zake nyingi zinakabiliwa na madhaŕa ya vita kati ya Urusi na Ukraine.

Nchini Nigeria, nchi yenye takriban watu milioni 215, wakulima wa mpunga wameonya kwamba mafuriko makubwa mwaka huu yanaweza kuongeza bei, kwani uagizaji wa mchele umepigwa marufuku ili kuongeza uzalishaji wa ndani.

Kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyochapishwa mwezi Septemba na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Nigeria tayari ni miongoni mwa nchi sita duniani zinazokabiliwa na hatari ya janga la njaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.