Pata taarifa kuu

Wanajeshi wa Côte d'Ivoire wazuiliwa Mali: Ujumbe wa ECOWAS wamaliza ziara yake Bamako

Ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ambao ulikuja kuomba kuachiliwa kwa wanajeshi 46 wa Côte d'Ivoire wanaozuiliwa tangu Julai 10, umekamilisha ziara yake. 

Wanajeshi wa Côte d'Ivoire huko Bouaké, Januari 13, 2017 (picha ya kumbukumbu).
Wanajeshi wa Côte d'Ivoire huko Bouaké, Januari 13, 2017 (picha ya kumbukumbu). Sia KAMBOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakuu wa Nchi za Gambia, Ghana, pamoja na mwakilishi wa Rais wa Togo hawakutoa tamko lolote. Lakini kulingana na habari yetu, hata kama hakuna taarifa rasmi kwa wakati huu, zaia hii inaweza kuzaa matunda.

Wakati wa mkutano na rais wa mpito Assimi Goïta, baadhi walibainisha kuwa mambo yanaweza "kwenda haraka", chanzo kilicho karibu na mazunumzo hayo kimebaini. Mshauri wa karibu wa Kanali Assimi Goïta pia amesema ana matumaini.

Ziara ya wajumbe wa taasisi ndogo ya kanda pia ilifuatiwa sana na kiongozi wa kidini mwenye ushawishi mkubwa wa eneo la Mali la Nioro. Pia aliingilia kati kuachiliwa kwa wanajeshi hao 46 wa Côte d'Ivoire, baada ya kupokea siku moja kabla ujumbe kutoka Côte d'Ivoire akiwemo mfanyabiashara wa Mali na mshauri anayesikilizwa sana na rais wa Côte d'Ivoire.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.