Pata taarifa kuu

Wanajeshi wa Côte d'Ivoire: Ujumbe wa upatanishi wa ECOWAS wawasili Bamako

Ujumbe wa ngazi ya juu uliotumwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) umewasili nchini Mali siku ya Alhamisi ili kujaribu kutatua mgogoro wa kidiplomasia kati ya Côte d'Ivoire na utawla wa kijehi, waandishi wa habari wameripoti.

Iliagizwa na viongozi wa nchi wanachama wa ECOWAS ambao walikutana katika mkutano wa kilele Septemba 22 kujaribu kutafuta njia ya mzozo kati ya Mali na Côte d'Ivoire.
Iliagizwa na viongozi wa nchi wanachama wa ECOWAS ambao walikutana katika mkutano wa kilele Septemba 22 kujaribu kutafuta njia ya mzozo kati ya Mali na Côte d'Ivoire. © wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Gambia Adama Barrow, kisha mwenzake wa Ghana Nana Akufo-Addo waliwasili kwa saa tofauti Alhamisi mchana kwenye uwanja wa ndege wa Bamako na kuelekea ikulu ya rais wa Mali.

Rais wa Togo Faure Gnassingbé, hapo awali alitangazwa kushiriki katika ujumbe huo, lakini amewakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje Robert Dussey. 

Robert Dussey, amethibitisha uwepo wake huko Bamako katika ujumbe kwa mwandishi wa shirika la habari la AFP.

Ujumbe huo unatakiwa kuondoka Alhamisi alasiri.

Iliagizwa na viongozi wa nchi wanachama wa ECOWAS ambao walikutana katika mkutano wa kilele Septemba 22 kujaribu kutafuta njia ya mzozo kati ya Mali na Côte d'Ivoire.

Bamako na Abidjan wako katika mzozo wa kidiplomasia kuhusu hatima ya wanajeshi 46 wa Côte d'Ivoire waliokamatwa Julai 10 walipowasili nchini Mali.

Wanajeshi hawa walikuwa, kulingana na Abidjan na Umoja wa Mataifa, wakishiriki katika ulinzi wa kikosi cha Ujerumani cha walinda amani nchini Mali. Lakini Bamako ilisema inawachukulia kama "mamluki" ambao walikuja kuhatarisha usalama wa taifa.

Utawala wa kijeshi wa Mali, ulio madarakani tangu 2020, ulionya kabla ya kupokea ujumbe huo kwamba hautakubali kulazimishwa suluhu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.