Pata taarifa kuu

CAR: Mahamat Said Abdel afutilia mbali mashtaka dhidi yake ICC

Kiongozi wazamani wa kundi la waasi nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Mahamat Said Abdel Kani, amekana mashtaka yanayomkabili katika mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za makosa ya uhalifu wa kivita, ICC.

Mahamat Said Abdel Kani akiingia katika chumba cha mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko Hague, Uholanzi, Jumatatu, Septemba 26, 2022. Mahamat Said Abdel Kani anatuhumiwa kwa "uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita".
Mahamat Said Abdel Kani akiingia katika chumba cha mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko Hague, Uholanzi, Jumatatu, Septemba 26, 2022. Mahamat Said Abdel Kani anatuhumiwa kwa "uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita". © AP Photo/Peter Dejong, Billard
Matangazo ya kibiashara

Kani mwenye umri wa miaka 52, anadaiwa kuwa kiongozi wa kundi la kiislamu la Seleka, linalotuhumiwa kutekeleza uhalifu dhidi ya binadamu hasa kwa waliokuwa wapinzani baada ya nchi hiyo kutumbukia katika machafuko mwaka 2013. 

Akizungumza mbele ya majaji wa mahakama hiyo mjini The Hague, Abdel Kani, amekana mashtaka dhidi yake akisisitiza kutokuwa na hatia ya makosa 7 ya uhalifu wa kivita na dhulma dhidi ya binadamu anayotuhumiwa. 

Waendesha mashtaka wanamtuhumu Kani, kuongoza kundi la wapiganaji wa Seleka kuvamia vituo vya polisi na kuwakamata wafuasi wa kiongozi wa zamani Francois Bozize na kisha kuwatesa. 

Katika kesi hiyo, wamo pia viongozi wawili wa zamani wa kundi la Anti Balaka, Patrice-Eduard Ngaissona na Alfred Yekatom. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.