Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Kesi ya kwanza dhidi ya mwanamgambo wa zamani wa Seleka kusikilizwa mbele ya ICC

Kesi ya Mahamat Saïd Abdel Kani, raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati inatarajiwa kufunguliwa Jumatatu hii, Septemba 26 mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huko Hague. Mmoja wa viongozi wa muungano wa SELEKA anayezuiliwa na ICC, 'Kanali Saïd' anatuhumiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Mahamat Saïd Abdel Kani mbele ya ICC, Oktoba 12, 2021.
Mahamat Saïd Abdel Kani mbele ya ICC, Oktoba 12, 2021. © Capture d'écran/CPI
Matangazo ya kibiashara

Inadaiwa kuwa uhalifu huo ulitekelezwa alipokuwa akiongoza Ofisi Kuu ya Kukandamiza Ujambazi (OCRB), baada ya Michel Djotodia kuchukua mamlaka mnamo mxezi Machi 2013.

Mahamat Said alikuwa kamanda na naibu chifu. Uhalifu unaodaiwa dhidi ya "Kanali" Said ulianzia majira ya baridi ya mwaka 2013, wakati muungano wa vyama kadhaa, SELEKA, ulipompindua Jenerali François Bozizé. Michel Djotodia alichukua usukani wa nchi na kuwazawadia baadhi ya makamanda wake, akiwemo Nourredine Adam, aliyeteuliwa kwenye wadhifa wa Usalama wa Umma. Akiwa chini ya amri yake, Mahamat Saïd, mshtakiwa, aliongoza wakati huo Ofisi Kuu ya Kuzuia Ujambazi (OCRB), kulingana na alivyoandika mwendesha mashtaka.

Wakati huo, mfuasi yeyote wa upinzani alilazimika kupigwa risasi. Rais aliyeondolewa madarakani, François Bozizé aliondoka kwenda Cameroon ili kufanya mageuzi ya wanajeshi wake, Anti-Balaka, na kuandaa mashambulizi ya kupambana na SELEKA. Ili "kuzuia upinzani na kusalia madarakani", SELEKA ilikabiliana na wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Bw. Bozizé. Watu kutoka kabila lake, Gbaya, walilengwa, kama Wakristo na baadhi ya maafisa na wananajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais, wanaoshukiwa kuwa watiifu kwa jenerali aliyetimuliwa. Katika miezi iliyofuata mapinduzi hayo, operesheni za upokonyaji silaha zililenga maeneo ya 4 na 7 ya Bangui, yanayojulikana kama wafuasi wa karibu wa Bozizé, njia panda ya PK9, na wilaya ya Boy Rabe, ambapo wanamgambo waliingia "nyumba kwa nyumba", kupora, kupiga , ubakaji, kuua. Wanamgambo wa SELEKA walikuwa wakisafiri kwa "gazi ndogo (pick-up) za aina ya kijeshi", zenye madirisha yenye rangi nyeusi, bila namba za kusajiliwa, na zikiwa na maandishi pembeni: "S'en fout la mort", au "Danger de mort, lawa , lawa [mtapatikana]". Wafungwa hao walikuwa wakipelekwa kwa CEDAD, Kamati ya Ajabu ya Kutetea Mafanikio ya Kidemokrasia na kwa OCRB, iliyoko mkabala na makao makuu ya polisi na karibu na ikulu ya rais huko Bangui.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.