Pata taarifa kuu

Wanajeshi watatu kati ya 49 wa Côte d'Ivoire wanaozuiliwa nchini Mali waachiliwa

Wanawake watatu ambao ni sehemu ya kundi la wanajeshi 49 wa Côte d'Ivoire waliokamatwa nchini Mali mnamo Julai 10 wameripotiwa kuachiliwa. Robert Dussey, mkuu wa diplomasia ya Togo, ametoa tangazo hilo Jumamosi jioni. Kesi ambayo Togo ni mpatanishi kati ya Bamako na Abidjan.

Mkuu wa Diplomasia ya Togo Robert Dussey (katikati) wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumamosi Septemba 3 akitangaza kuachiliwa kwa wanajeshi watatu wa kikosi cha Côte d'Ivoire wanaozuiliwa nchini Mali.
Mkuu wa Diplomasia ya Togo Robert Dussey (katikati) wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumamosi Septemba 3 akitangaza kuachiliwa kwa wanajeshi watatu wa kikosi cha Côte d'Ivoire wanaozuiliwa nchini Mali. © Peter Sassou Dogbe/RFI
Matangazo ya kibiashara

Tangazo rasmi limetolewa mjini Lomé, nchini Togo, Jumamosi jioni wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo bendera tatu za Togo, Mali na Côte d'Ivoire zilionekana kwenye madawati.

Togo, nchi ya upatanishi, inajitahidi watu hawa 49 waweze kuachiliwa kupitia. Leo hasa, mazungumzo yamekuwa yakiendelea.

Kutoka kwa vyanzo vilivyo karibu na faili hili, mjini Abidjan kama vile Bamako, inafahamika kuwa juhudi kubwa zinaendelea kusogeza mbele faili. Wanajeshi hawa 49 wa Côte d'Ivoire wamezuiliwa nchini Mali tangu Julai 10.

Mali inawatuhumu kuwa "mamluki". Abidjan, ambayo inaomba kuachiliwa kwao, inahakikisha kwa upande wake kwamba walikuwa kwenye misheni ya Umoja wa Mataifa, kama sehemu ya shughuli za usaidizi wa vifaa kwa MINUSMA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.